Online

Wednesday, December 26, 2012

Safu za milima mirefu barani AfricaOrodha hii ya kumi bora ya safu za milima mirefu barani Africa imetawaliwa na vilele vya milima kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Ethiopia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Zingatia: orodha hii haijapangwa kutokana na urefu wa mlima ila imepangwa kwa lengo la kuiainisha milima hiyo. Mlima mrefu zaidi barani Afrika unabaki kuwa ni mlima Kilimanjaro ukifuatiwa na mlima Kenya.
Milima Bale
Milima ya Bale ipo nchini Ethiopia, na inapatikana katika hifadhi ya taifa ya Bale, inajumuisha mlima Tullu Demtu ambao ni mlima wa pili kwa urefu nchi Ethiopia na mlima Batu.
Milima hii ni maarufu kwa kuhidahi wanyama wakali hasa mbwa mwitu, pia aina nyingine za mamalia zipatazo 60 na aina 260 za ndege. Katika milima hii hufanyika shughuli za kupanda milima hiyo, kuvua samaki na kuwinda ndege.
Milima Rwenzori
Milima ya Rwenzori hujulikana pia kwa jina la milima ya Mwezini, inapatikana katika mpaka wan chi za Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Vilele virefu zaidi katika safu hii vimefunikwa na barafu na daima hufunikwa na mawingu. 
Makampuni kadhaa hufanya safari katika milima hii mara 10 kwa siku. Wapandaji maalumu hupanda hadi katika kilele cha Margherita katika mlima Stanley, ambao ni mlima namba tatu kwa urefu barani Africa ukiwa na urefu wa mita 5109.
Toubkal Atlas
Toubkal ni kilele kirefu zaidi katika safu ya milima ya Atlas ambayo hupatikana nchini Morocco katika hifadhi ya taifa ya Toubkal. 
Safu hii inajumuisha nchi za Morocco, Tunisia na Algeria. Wapandaji huweza kupanda kwa msaada wa waongozaji wake na wabeba mizigo.
Mlima Guna
Mlima Guna, unapatikana katika uwanda wa juu nchini Ethiopia, ni mlima mrefu katika ukanda wa Debub Gondar. 
Mlima huu ni chanzo cha maji ya mito ya Erib na Beshlo. Miji ambayo iko karibu na mlima huu ni Debre Tabor na Gondar.
Mlima Meru
Mlima Meru unapatika nchini Tanzania na uko kilomita 70 kutoka mlima Kilimanjaro. Mlima huu umezungukwa na mbuga na msitu wa hifadhi ya taifa ya Arusha, ambayo ina wanyama kama vile tumbili, chui na karibu aina 400 za ndege.
Mlima Meru waweza kuoneka kutoka mlima Kilimanjaro wakati wa mchana tulivu. Mlima huu unaweza kupandwa kwa siku tatu hadi nne, huku wapandaji wakipumzika katika vibanda maalumu.
Mlima Elgon
Athari za volcano katika mpaka kati ya nchi za Uganda na Kenya imesababisha kupatikana kwa vilele vitano. Mlima huu una mapango kadhaa, lakini pango maarufu ni lile lijulikanalo kama Kitum. Pango hili lina upana wa mita 60+ na kina cha zaidi ya mita 200, huwavutia tembo ambao hupenda chumvi ipatikanayo katika kuta za pango hilo.
Shughuli zifanywazo mbali na kupanda mlima huu ni kambi, kuangalia wanyama na kuangalia ndege mbalimbali wanaopatikana katika eneo linalozunguka mlima. Muda mzuri wa kupanda mlima ni katika kipindi cha kiangazi (June-August au December - February).
Mlima Kilimanjaro
Mlima Kilimanjaro ndiyo mlima mrefu zaidi barani Africa, wakati kilele cha Uhuru/Kibo ni mlima mrefu ulio huru duniani. Mlima Kilimanjaro hujulikana pia kuwa ndiyo mlima maarufu zaidi barani Africa.
 Huwachukua watalii siku saba had inane kuupanda mlima huu. Mlima huu unapatikana ndani ya hifadhi ya taifa ya Kilimanjaro.
Milima Virunga
Safu ya milima Virunga hujumuisha milima minane ya volcano katika mpaka wa nchi za Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Uganda. Milima miwili ya volcano, Mlima Nyiragongo na Mlima Nyamuragira ni hodari, ambapo milipuko imewahi kutokea katika miaka ya 2006 na 2010. 
Milima Virunga ni nyumba masokwe wa aina mbili waliobakia ambao ni hatari. Dian Fossey, ambao ile movie ya Gorillas in the Mist imeigiziwa, alifanya utafiti katika milima Virunga nchini Rwanda. Kupanda kilele cha Karisimbi, ambacho ni kilele kirefu katika safu hii, ni siku mbili kwa mpandaji aliye na afya zake.
Mlima Kenya
Mlima mrefu zaidi katika nchi ya Kenya na mlima unaoshika namba mbili kwa urefu barani Africa ni mlima Kenya. Nchi hii ya Afrika Mashariki imechukua jina lake kutoka katika mlima huu. Kama ilivyo kwa milima mingine barani Africa, mito ya barafu katika mlima Kenya hupatikana pia.
 Kuna aina tofauti za wanyama wapatikanao katika mtelemko hafifu wa mlima huu, ikiwamo tumbili, nungunungu, na tembo. Kilele cha Lenana ni rahisi kukifikia tofauti na Nelion na Batian ambacho ni ngumu kupanda.
Milima Semien  
Milima Semien inapatikana katika hifadhi ya taifa ya Semien huko nchi Ethiopia. Kilele kirefu zaidi katika safu hii ni Ras Dashen. Kihistoria milima hii ilikuwa ni makazi ya wayahudi wa Ethiopian. 
Hadi kuufikia mlima Ras Dashen huchukua takriban siku nane na hulazimika kupitia katika mabonde ya Imet Gogo na Emsheha kwa msaada wa waongozaji, wabeba mizigo na punda.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.