Online

Friday, May 3, 2013

20 bora ya nchi masikini zaidi duniani


Ni nchi gani masikini zaidi duniani? Ifuatayo ni orodha ambayo imechapichwa katika mtandao wa Wikipedia kutoka Shirika la Fedha Ulimwenguni (IMF) mwaka 2011 ikizingatia pato la ndani la nchi huzika. Tangu mwaka 1970, kumekuwa na taarifa mbalimbali juu ya nchi zinazoendelea. Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa linalojihusisha na maendeleo ya watu iliyotoka mwaka 2010, muda wa kuishi katika nchi zinazoendelea imeongezeka kutoka miaka 59 mwaka 1970 hadi miaka 70 mwaka 2010. 
Idadi ya watoto waliotakiwa kwenda shule nayo imeongezeka kutoka 55% hadi 70% katika shule zote za msingi na sekondari. Pia katika kipindi cha miaka 40 iliyopita, pato la taifa liliongezeka mara mbili kwa zaidi ya dola 10,000. Nchi masikini zinainuliwa na nchi tajiri, lakini siyo nchi zote zinakuwa haraka kiuchumi. Kwa mfano, baadhi ya nchi zipatikanazo katika jangwa la Sahara zinakuwa kidogo au hazikui kabisa, hii hasa ni kutokana na uwepo wa ugonjwa hatari wa UKIMWI na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Orodha kamili ya 20 bora ya nchi masikini zaidi duniani:
#1. Congo, Democratic Republic of the
Pato la taifa: dola 348 (kwa mwaka 2011)
Hii haichanganywi na nchi jirani ya Jamhuri ya Congo, nchini Jamhuri ya kidemkrasia ya Congo imekuwa masikini na inaongoza katika orodha hii duniani kwa mwaka 2010. Nchi hii mara ya kwanza ilifahamika kwa jina la Zaire mpaka mwaka 1997. Ni nchi kubwa duniani ambayo hutumia lugha ya kifaransa kama lugha maalumu – na nchi hii ina watu milioni 6 zaidi ya watu wa Ufaransa (71 million nchini D.R Congo wakati Ufaransa ina watu 65 million). Vita ya pili nchini humo imeanza mwaka 1998 ambayo imeididimiza zaidi nchi hiyo. Ni vita ambayo imehusisha wanajeshi wa kigeni (kutoka nchi za kigeni 7) ni vita ambayo ni mbaya zaidi ukiiondoa Vita kuu ya Pili ya Dunia (World War II) – mwaka 2008 vita vya pili vya Congo na mpaka hivi vinavyoendelea, vimegharimu maisha ya zaidi ya watu 5.4 million.
#2. Liberia
Pato la taifa: dola 456 (mwaka 2011)
Nchi ya Liberia ni moja ya nchi chache za kiafrika ambazo hazijatawaliwa na watu wa Ulaya Europe. Badala yake, nchi hii ya Liberia ilikuwa ni makao ya watumwa waliorudishwa kutoka nchini Marekani baada ya kusitishwa biashara ya watumwa. Watumwa hawa ndiyo wakatumia kisomo chao kisha wakaanzisha serikali ambayo kwa kila namna inafanana na ile ya Marekani. Mwaka 1980 aliyekuwa rais wan chi hiyo alipinduliwa kisha kikafuata kipindi cha kupotea kwa amani na vita vya ndani. Baada ya mauaji ya mamia kwa maelfu ya watu, mwaka 2003 mpango wa amani ambao ulipelekea uchaguzi huru na wa amani mwaka 2005 ulisainiwa. Leo, Liberia inakabiliwa na athari za vita vya ndani hata kusababisha uchumi wake kuyumba kwa kiasi kikubwa, ikiwa na zaidi ya 85% ya watu wake wakiishi chini ya dola moja kwa siku.
#3. Zimbabwe
Pato la taifa: dola 487 (mwaka 2011)
Serikali ya Zimbabwe ilitoa taarifa za kibenki ambayo ilionesha dola 100 trillion mnamo mwezi January, 2009. Pia kutokana na matatizo ya kiuchumi, umri wa kuishi nchi humo ni ndogo zaidi duniani ikiwa ni miaka 37 kwa wanaume na miaka 34 kwa wanawake. Moja ya tatizo la vifo vya mapema ni kuwa 20.1% ya watu wake wana maambukizi ya ugonjwa hatari wa UKIMWI. Suala la afya katika nchi hii halijaimarishwa.
#4. Burundi
Pato la taifa: dola 615 (mwaka 2011)
Nchi ya Burundi inafahamika kutokana na vita vya ukabila na vya wenyewe kwa wenyewe.  Burundi haina jata mara moja kipindi chochote cha amani hata kusababisha kuwa nafasi ya nne katika orodha hii. Haina Jiografia nzuri, mfumo mbovu wa serikali, hakuna uhuru wa uchumi, uhaba wa shule hata kusababisha kuwa na wasomi wachache, maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI. Inakisiwa kuwa 80% ya warundi wanaishi katika umasikini mkubwa na kwa mujibu wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, 57% ya watoto walio chini ya umri wa miaka 5 hawapati chakula bora.
#5. Eritrea
Pato la taifa: dola 735 (mwaka 2011)
Nchi hii imeathiriwa zaidi na ukoni wa Italia katika karne ya 19. Kutokana na kuwa katika ule mfereji wa Suez mchi hii imejikuta ikitawaliwa na Italia mwaka mmoja tu tangu kufunguliwa kwake mwaka 1869 na kwa sababu hiyo hiyo Uingereza ikaitawala mwaka 1941. Leo hali ya uchumi wa Eritrea haijaimarishwa na pato la taifa limekuwa kwa 1.2% kati ya mwaka 2005 na 2008; mwaka 2009 pato lilikuwa kwa wastani wa 2.0%.
Nchi nyingine ni;
#6. Jamhuri ya Afrika ya Kati
#7. Niger
#8. Sierra Leone
#9. Malawi
#10. Togo
#11. Madagascar
#12. Afghanistan
#13. Guinea
#14. Mozambique
#15. Ethiopia
#16. Mali
#17. Guinea-Bissau
#18. Comoros
#19. Haiti
#20. Uganda

1 comment :

  1. jamani maendeleo ya nchi ni wananchi wenyewe kila mtu ajitahidi kufanya kazi na kujituma na pia tuwe wabunifu na kujiajiri wenyewe serikali na viongozi ni ziada tu.

    ReplyDelete

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.