Online

Tuesday, December 30, 2014

Sports News: Cristiano Ronaldo vs Lionel Messi: Wachezaji wawili wenye kiwango cha hali ya juu Duniani goli-kwa-goli na rekodi-kwa-rekodi mwaka 2014  • Wote Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wamekuwa na miaka yenye mafanikio katika soka
  • Messi aliisaidia Argentina kufika fainali ya Kombe la Dunia, lakini walipoteza kwa Ujerumani na kupewa tuzo ya Mchezaji bora wa mashindano
  • Akiwa na Barcelona, amevunja rekodi ya mabao ya La Liga na Champions League
  • Lakini walishindwa kutwaa taji hata moja, walikosa taji la La Liga na Europe
  • Mfungaji-huru Ronaldo aliisaidia Real kutwaa taji la 10 la Champions League
  • Akaisaidia kushinda Kombe la Copa del Rey, European Super Cup na Klabu Bingwa Dunia
  • Lakini Ureno iliishia hatua ya makundi kwenye Kombe la Dunia 
Ni uhasama mkubwa uliopo baina ya wachezaji wawili katika soka kuwahi kutokea na mwaka 2014 ulishuhudia Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wakiendelea kuweka ugumu kwa wapenzi wa soka juu ya nani zaidi ya mwingine.
Mabao yamehuhudiwa na rekodi kibao zikavunjwa ambapo Mreno na Muargentina walithibitisha ubora wao katika kunyanyasa kuta za timu pinzani.
Katika kusherehekea mafanikio yao, blog hii inakwenda nawe mwezi kwa mwezi kuanzia Januari hadi Disemba kuangalia nini wachezaji hawa mahiri ulimwenguni walikifanya mwaka huu 2014. 
 JANUARI
6: Real Madrid yacheza mechi ya kwanza kufuatia mapumziko ya kipindi cha baridi, Ronaldo alifunga mara mbili katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Celta de Vigo na kufikisha mabao 400 tangu alipoanza kucheza soka la kulipwa katika michezo 653 ya klabu na timu ya taifa. Aliyatoa mabao hayo kwa mkali wa Ureno Eusebio, ambaye alifariki siku mbili nyuma.
8: Messi arejea dimbani baada ya kuwa majeruhi ambayo yalimuweka nje tangu Novemba na kufunga mara mbili katika mchezo wa Copa del Rey ambapo Barcelona ilishinda 4-0 dhidi ya Getafe.
Messi akishangilia kurejea dimbani baada ya kuwa majeruhi na kufunga dhidi ya Getafe kwenye mchezo wa Copa del Rey mapema Januari 
11: Messi atokea benchi kipindi cha pili lakini alishindwa kuisaidia Barcelona kupata ushindi dhidi ya Atletico Madrid. Mechi hiyo ilimalizika kwa matokeo ya 0-0. Barcelona yabaki kileleni, lakini tofauti ya mabao inawafanya wakae chini ya Atleti.
13: Ronaldo amshinda Messi katika tuzo ya FIFA Ballon d'Or, akivunja rekodi ya muargentina huyo kuwaa tuzo mara nne mfululizo. Mreno huyo alipat pointi 1,365, Messi akapata pointi 1,205 na mshindi wa tatu Franck Ribery alipata pointi 1,127. Ronaldo amwaga machozi wakati anapokea tuzo hiyo mjini Zurich.
Ronaldo akijifuta machozi baada ya kushinda tuzo ya Ballon d'Or kwa kuwa Mchezaji Bora Duniani mjini Zurich mwezi Januari 
Ronaldo akimuangalia hasimu wake katika soka Messi akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari kuelekea sherehe za utoaji tuzo ya Ballon d'Or 
 Messi, akiwa katika suti nyekundu akiwaili kwenye sherehe za tuzo ya Ballon d’Or akiwa na mpenzi wake Antonello Roccuzzo
Ballon d'Or: Messi akitoa pongezi kwa Cristiano Ronaldo
15: Ronaldo athibitisha ubora wake kuwa ni Mchezaji Bora wa Dunia kwa kufungua karamu ya mabao ambapo Real ilishinda 2-0 dhidi ya Osasuna kwenye mchezo wa Copa del Rey.
16: Hawezi kusubiri, Messi alifunga mara mbili katika mchezo ambao Barcelona ilishinda kwa uwiano wa 6-0 dhidi ya Getafe kwenye hatua ya 16 ya Copa del Rey.
18: Bao la ufunguzi la Ronaldo dakika ya 10 dhidi ya Real Betis linaifanya Real kushinda 5-0 na kufikisha pointi 50 kwenye La Liga.
25: Real walipiga kwa juhudi na bao la Ronaldo dakika ya 56 linaipa matumaini na kushinda 2-0 nyumbani dhidi ya Granada.
Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia Real Madrid kwenye mchezo dhidi ya Granada mwishoni mwa Januari

FEBRUARY
1: Messi afunga bao la kusawazisha kwa mkwaju wa penalty kipindi cha pili lakini Barcelona wanakufa 3-2 nyumbani dhidi ya Valencia, hii inawaruhusu Atletico kusogea kileleni kwa pointi tatu kuelekea ubingwa wa La Liga.
2: Ronaldo anatolewa kwa kadi nyekundu kwa mara ya saba katika kipindi chake cha soka huku Real ikisimamishwa kushinda mechi mfululizo – ilishinda mechi nane mfululizo lakini katika mchezo huo ililazimishwa sare ya 1-1 na Athletic Bilbao. Ronaldo alinyoosha mikono yake katika mabishano na Carlos Gurpegi na kuoneshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja, akafungiwa mechi tatu.
Ronaldo akimuangalia mwamuzi baada ya kuoneshwa kadi nyekundu na mwamuzi Ayza Gamez kwenye mchezo dhidi ya Athletic Bilbao
9: Mabao mawili ya Messi yaliisaidia Barca kushinda 4-1 dhidi ya Sevilla, kazi ilifanywa na Alexis Sanchez na Cesc Fabregas waliopiga mashuti yaliyolenga lango.
11: Kwa sababu kadi aliyopewa Ronaldo haikuhusu mechi za Copa del Rey, alifunga mara mbili kwa penalty katika mchezo wa marudiano ya nusu fainali dhidi ya Atletico Madrid. Ushindi wa mabao 2-0 ulikamilisha jumla ya mabao a 5-0 na kuingia kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Barcelona. Penalty yake ya dakika ya saba inamaana Ronaldo amefunga katika kila dakika kwenye dakika 90 kwenye mechi za soka.
Ronaldo akifunga penalty na kuisaidia Real kushinda dhidi ya Atletico kwenye nusu fainali ya Copa del Rey
15: Messi alifunga mara mbili dhidi ya Rayo Vallecano katika ushindi wa 6-0 na kumzidi Alfredo di Stefano na kufungana na Raul katika nafasi ya tatu ya ufungaji wa muda wote kwenye historia ya La Liga akiwa na mabao 228.
18: Messi afunga kwa penalty kwenye mchezo wa awali wa Champions League hatua ya 16 dhidi ya Manchester City. Zikiwa hazijafungana, aliangushwa chini na Martin Demichelis wakati wakiwania mpira uliopigwa na Andres Iniesta. Mwamuzi Jonas Eriksson alitoa penalty na kumtoa nje Demichelis. Messi hakufanya hiyana dhidi ya City na hadi mwisho Barca ilishinda 2-0.
Messiakifunga kwa penalty dhidi ya Manchester City katika mchezo wa awali wa Champions League hatua ya mtoano 
 Barcelona ilishinda 2-0 kwenye dimba la Etihad
22: Messi afanya juhudi kwenye dimba la Anoeta, lakini Barcelona iliangamia kwa 3-1 kutoka kwa Real Sociedad ambapo iliwaruhusu Real Madrid kukaa kileleni.
26: Ronaldo afunga mara mbili wakati Real Madrid ikielekea kwenye kuusaka ubingwa wa Champions League na kuichapa Schalke 6-1 mjini Gelsenkirchen. Mabao yake hayo yalikuwa na maana kuwa Ronaldo alikuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao 10 au zaidi katika mashindano matatu mfululizo ya Champions League.

MARCH
2: Barcelona yaondoa machungu kutoka kwa Sociedad kwa kushinda 4-1 dhidi ya Almeria - Messi alifunga bao la pili. Katika siku hiyo hiyo, Ronaldo alifunga bao la kusawazisha katika dakika za lala salama ambapo Madrid derby ikimalizika kwa sare ya 2-2. Zilikuwa zimebakia dakika nane ambapo Ronaldo alimalizia krosi ya Daniel Carvajal na kugawana pointi. Hali hiyo ilipelekea msimamo kuwa hivi: Real Madrid 64pts, Barcelona 63pts, Atletico Madrid 61pts.
5: Ronaldo afunga mara mbili kuanza harakati zake za kimataifa akiwa na Ureno ambapo waliichakaza Cameroon 5-1 katika mechi ya kirafiki. Mabao hayo yanamfanya kufikisha mabao 49, na kumfanya kuwa mfungaji bora wa muda wote wan chi hiyo. Katika usiku huo huo, Messi aliichezea Argentina katika mchezo uliomalizika kwa sare ya bila kufungana dhidi ya Romania mjini Bucharest.

Ronaldo akishangilia mojakati ya mabao yake katika mchezo ambao Ureno ilishinda 5-1 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Cameroon 
8: Messi na Barcelona wapata pigo linguine kuelekea ubingwa baada ya kupoteza 1-0 kutoka kwa Valladolid.
9: Bao la dakika ya 11 la Ronaldo linaiweka Real kwenye njia nzuri kuelekea ubingwa baada ya kushinda 3-0 dhidi ya Levante kwenye dimba la Bernabeu.
12: Messi aendelea tena kuitesa Manchester City baada ya bao lake kwenye dimba la Nou Camp kuipa ushindi wa 2-1 kwenye mchezo wa marudiano hivyo Barcelona walishinda 4-1 kwa mechi zote mbili. Messi aliwahadaa mabeki wa City na kumalizia kazi nzuri ya Cesc Fabregas. Ushindi huo una maana kuwa Barcelona inasonga mbele kuingia hatua ya nane bora ya Champions League kwa misimu saba mfululizo.
 Messi kifunga mbele ya Joe Hart na kuisaidia Barcelona kuishinda Manchester City
15:Katika kuifungia Real bao la ushindi dhidi ya Malaga, Ronaldo anakuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao 25 katika misimu mitano mfululizo.
16: Hat-trick ya Messi katika ushindi wa 7-0 dhidi ya Osasuna inamfanya kuwa nyuma ya Paulino Alcantara katika ufungaji wa muda wote kwenye klabu ya Barcelona kwenye mashindano yote ambapo hata mabao ya mechi za kirafiki yakijumuishwa.
18: Mabao mawili ya Ronaldo dhidi ya Schalke katika mchezo wa marudiano ya Champions League hatua ya mtoano yanamfanya kufikisha mabao 12 kwenye msimu mmoja wa Champions League. Pia inamfanya kuwa nyuma ya rekodi ya mabao 14 ya Messi kwa bao moja, aliyoiweka msimu wa 2011-12.
Ronaldo akimpa tano Gareth Bale baada ya kufunga dhidi ya Schalke kwenye mchezo wa marudiano ya Champions League hatua ya 16
23: Nyota hao wawili walikutana uso-kwa-uso kwenye Clasico kwenye dimba la Bernabeu ambapo kulikuwa na matokeo yasiyotarajiwa. Messi alifunga hat-trick, ikijumuisha mabao mawili ya penalti, na kujihakikishia ushindi wa 4-3 na kuifanya Barcelona kuutikisa ubingwa. Ronaldo alifunga kwa penalty lakini akamaliza kwa kipigo. Mabao ya Messi yalishuhudia yakimuweka juu ya Di Stefano na kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Clasico na kumzidi Hugo Sanchez na kuwa nafasi ya pili ya ufungaji bora wa muda wote kwenye historia ya La Liga.
26: Messi afunga mechi ya nne mfululizo ambapo Barcelona ilishinda 3-0 dhidi ya Celta de Vigo. Haikuwa habari njema kwa Real, ambayo ilichapwa 2-1 na Sevilla licha ya Ronaldo kufunga bao la kuongoza.
29: Messi tena athibitisha ubora wake baada ya kufunga kwa penalty dakika ya 77 kwenye mchezo wa Catalan derby dhidi ya Espanyol. Ronaldo alifungua karamu ya mabao kwenye ushindi wa 5-0 ambao Real iliichakaza Rayo Vallecano, ikimaanisha amesawazisha rekodi ya Messi ya kufunga mabao 10 mfululizo kwenye mashindano yote.
Ronaldo anaweza kutizama pekee wakati Messi akifunga hat-trick kwenye mchezo ambao Barcelonailishinda 4-3 kwenye dimba la Bernabeu 

APRIL
1: Barcelona na Atletico Madrid watoka sare ya 1-1 Nou Camp katika mchezo wa awali wa Champions League hatua ya robo fainali, huku Neymar akisawazisha baada ya Diego kufunga bao la kuongoza. Thibaut Courtois afanyakazi nzuri kwa kuokoa hatari.
2: Katika mchezo wake wa 100 wa Champions League kwenye mchezo wa Real Madrid dhidi Borussia Dortmund, bao la Ronaldo dakika ya 57 yahitimisha karamu ya mabao 3-0. Aifikia rekodi ya Messi ya mabao 14 kwenye Champions League na kujiunga na Di Stefano katika nafasi ya pili ya ufungaji bora wa muda wote kwenye klabu katika mashindano ya Ulaya kwamabao 49. Raul aendelea kuongoza kwa kuwa na mabao 66. Ronaldo pia anakuwa mchezaji wa kwanza kufunga kwenye mechi nane mfululizo za Champions League. Hata hivyo, anatolewa nje dakika 10 kabla ya mchezo kumalizika nah ii ilimaanisha atakosa mechi nne.
Ronaldo akimzidi maarifa mlinda mlango wa Borussia Dortmund Roman Weidenfeller na kufunga bao kwenye dimba la Bernabeu mwezi April
5: Mabao mawili ya Messi yaisaidia timu yake kushinda 3-1 nyumbani dhidi ya Real Betis ambapo Barcelona yawafukuzia vinara Atletico. Baada ya mechizo ya mwishoni mwa wiki, Barca yawa nyuma kwa pointi moja.
9: Matumaini ya Messi kushinda taji la nne la Champions League yamalizwa na Atletico, ambayo ilishinda mchezo wa marudiano wa Champions League hatua ya robo fainali kwa bao 1-0 shukrani kwa bao la Koke dakika za mapema na timu hiyo ilitinga hatua ya nusu fainali kwa uwiano wa mabao 2-1.
12 Kutoka kwenye hali mbaya hadi mbaya zaidi kwa Barca, ambao walishangazwa baada ya kuchapwa 1-0 na Granada.
16: Licha ya kukosekana kwa Ronaldo, Real Madrid yashinda mchezo wa fainali ya Copa del Rey dhidi ya Barcelona ama Clasico Copa del Rey kwa mabao 2-1. Mchezo huo ulipigwa kwenye dimba la Mestalla mjini Valencia ulishuhudia bao la dakika ya tano kutoka kwa Gareth Bale. Ni mara ya pili kwa Ronaldo kushinda mashindano hayo.
20: Messi afunga bao la ushindi kwa Barcelona kwenye dimba la Camp Nou kwa kuichapa Athletic Bilbao 2-1. Hii ilikuwa baada ya Artiz Aduriz kufunga bao la kuongoza, lakini Pedro na Messi walifunga mabao ndani ya dakika mbili na miamba hiyo ya Catalanwakijaribu kukaa sawa baada ya kupoteza kwenye fainali ya Copa del Rey.
Messi akishangilia na Andres Iniesta baada ya kumalizika mchezo wao dhidi ya Athletic Bilbao 
23: Ronaldo arejea baada ya kusumbuliwa na majeraha ya paja na kumaliza dakika 73 za Real kuibuka na ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa awali wa nusu fainali ya Champions League dhidi ya Bayern Munich. Aliisaidia timu yake kulinda bao lao lililofungwa na Karim Benzema dakika ya 19.
26: Ronaldo alicheza dakika 60 wakati wa mchezo ambao Real ilishinda mabao 4-0 dhidi ya Osasuna lakini aliweza kufunga mara mbili katika dakika hizo. Walipata pointi, Carlo Ancelotti kwa busara alimpa usiku uliopita kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Bayern. Magoli hayo yalikuwa magoli 100 na 101 ya ligi kwenye dimba la Bernabeu.
27: Messi alifunga kunako dakika saba kabla ya kumalizika katika mchezo dhidi ya Villarreal ambapo Barcelona walikuwa nyuma ya Villarreal. Walikuwa nyuma kwa mabao mawili ndani ya dakika 55 lakini Villarreal walijifunga mara mbili kabla ya Messi kufunga bao la ushindi. Licha ya hii, Barcelona waliwachwa nyuma kwa pointi nne na vinara Atletico.
29: Kwa ajili ya kupata matokeo bora ya mwaka, Ronaldo alifunga mara mbili katika mchezo ambao Real iliichapa Bayern 4-0 katika dimba la Allianz Arena na kutinga hatua ya fainali ya Champions League. Baada ya Sergio Ramos kufunga mara mbili kwa kichwa, Ronaldo akafunga bao la tatu akiunganisha krosi ya Bale likiwa bao lake la 48 la msimu. Kasha, dakika ya 89, Ronaldo alifunga bao la nne kwa mpira wa adhabu na kufikisha mabao 16 ya msimu kwenye Champions League, akiivunja rekodi ya mabao 14. Sasa ana rekodi ya mabao 33 kwenye hatua ta mtoano, mawili zaidi ya Messi. Pia afikisha magoli hamsini ya Ulaya akiwa na Real.
Ronaldo akimtungua Manuel Neuer wakati wa mchezo wa nusu fainali ya Champions League dhidi ya Bayern Munich 
 Ronaldo akifunga kwa adhabu kwenye mchezo dhidi ya Bayern

MAY
3: Messi anafunga tena lakini Barcelona wanalazimishwa sare ya 2-2 dhidi ya Getafe nyumbani, inaharibu mipango yao ya kutwaa taji.
4: Ronaldo anaokoa pointi katika mchezo ambao Real ililazimishwa sare ya 2-2 nyumbani na Valencia kwa kufunga katika dakika za lala salama. Inakuwa njia inayomfikisha kutwaa tuzo ya Mfungaji Bora wa LFP kwa msimu wa 2013-2014.
7: Nafasi ya Real kutwaa taji inakufa baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Valladolid.
11: Barcelona yalazimishwa sare ya 0-0 dhidi ya Elche, ikiwawacha pointi tatu nyuma ya Atletico kuelekea taji.
16: Messi akubali mkataba mpya na Barcelona.
17: Jaribio la Barcelona kuiba taji la La Liga kutoka kwa Atletico lamalizwa kwa sare ya 1-1 na vinara katika mchezo wa mshindi anatwaa zote kwenye dimba la Nou Camp. Licha ya Alexis Sanchez kufunga bao la kuongoza dakika ya 33, bao la kusawazisha la Diego Godin mapema kipindi cha pili linawahakikishiautaji Atletico. Barca walijaribu kila mbinu kuhakikisha wanashinda lakini hawakuweza na Atleti wakatwaa taji lao la kwanza tangu katikati ya 1990. Msimamo wa mwisho ulisomeka: Atletico 90pts, Barcelona 87pts, Real Madrid 87pts.
Mlinda mlango wa Atletico Thibaut Courtois akishangilia katika dimba la Nou Camp baada ya kutawazwa mabingwa
Msimu wa Messi unamalizika bila mafanikio licha ya kushinda taji moja la Super Cup. Anamaliza kampeni akiwa na mabao 41 na kutengeneza 15 katika mashindano yote. Mabao yake 28 hayatoshi kumpa tuzo ya Pichichi kwa ufungaji bora. Ronaldo aitwaa kwa mabao 31.
24: Ronaldo anakuwa Bingwa wa Ulaya kwa mara ya pili katika maisha yake ya soka na kuisaidia Real Madrid kumaliza ukame wa miaka 14 wa kusubiri 'Decima', taji lao la 10 la Champions League. Katika usiku mzuri kwenye dimba la Estadio da Luz in Lisbon, Real yatoka nyuma dhidi ya mahasimu wao kutoka jiji moja Atletico na kushinda 4-1 katika muda wa ziada. Ronaldo aweka historia kwa penalty ya dakika ya 120 na kuondoa jezi yake na kutunisha misuli katika kusherehekea na kupigwa picha ambayo imekuwa gumzo mwaka 2014.
Ni bao lake la 17 la Champions League katika msimu huo, na kumfanya kuwa mfungaji bora kwa mara ya pili mfululizo. Anamaliza msimu kwa kufunga mabao 51 katika mechi 47 kwenye mashindano yote. Anachangia tuzo ya ufungaji bora Ulaya na mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez.
Ronaldo akishangilia kwa kuvua jezi na kutunisha misuli baada ya kuifungia Real bao la nne kwenye mchezo wa fainali ya Champions League dhidi ya Atletico  
Wachezaji wa Real Madrid wakishangilia baada ya kutwaa Kombe la Ulaya kwa kuwachapa majirani zao Atletico mjini Lisbon 

JUNE
4: Messi anacheza, lakini hafungi, katika mchezo ambao Argentina ilishinda 3-0 dhidi ya Trinidad and Tobago, mchezo wao wa kwanza wa maandalizi kwa ajili ya Kombe la Dunia nchini Brazil.
6: Akipambana na maumivu ya goti, Ronaldo akaa nje katika mchezo wa maandalizi ya Kombe la Dunia dhidi ya Mexico. Analazimishwa kufanya mazoezi ili awe fit kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia.
7: Messi anaifungia Argentina bao la pili katika mchezo wa kirafiki na kushinda 2-0 dhidi ya Slovenia.
11: Ronaldo arejea dimbani kwa mafanikio ambapo Ureno iliichapa Jamhuri ya Ireland 5-1 katika mchezo wao wa mwisho wa maandalizi ya Kombe la Dunia. Alicheza dakika 66 mjini New Jersey.
15: Messi aanza kuonesha maajabu kwenye dimba la Maracana, afunga katika mchezo wao wa ufunguzi wa Kombe la Dunia ambao Argentina ilishinda 2-1 dhidi ya Bosnia-Herzegovina. Wanaongoza baada ya dakika ya tatu wakati mlinzi Sead Kolasinac alijifunga kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Messi. Kasha dakika ya 65, Messi anagongeana na Gonzalo Higuain, awalamba chenga mabeki wawili na kufunga bao. Bao hilo, linamaliza dakika 623 za Messi na kufunga bao la 39 kwa Argentina. Mara ya mwisho kufunga ilikuwa dhidi ya Serbia na Montenegro Juni 16, 2006.
Messi akiwatoka walinzi wa Bosnian na kuifungia Argentina kwenye mchezo wa Kombe la Dunia 
 Messi akishangilia kwenye dimba la Maracana baada ya Argentina kushinda
16: Ronaldo akutana na dakika 90 mbaya katika maisha yake ya soka baada ya Ureno kutandikwa mabao 4-0 na Ujerumani katika mchezo wao wa ufunguzi wa Kombe la Dunia hatua ya makundi. Ronaldo atoka kappa, Thomas Muller afunga hat-trick huku Pepe akioneshwa kadi nyekundu kwa kumpiga kichwa Muller. 


Ronaldo akipigwa na butwaa baada ya Ureno kukung’utwa mabao 4-0 na Ujerumani
21: Messi afunga tena ambapo Argentina yapata ushindi wa 1-0 dhidi ya Iran. Ikionekana kuwa mchezo huo utamalizika kwa sare ya bila kufungana, dakika za lala salama, Messi apigwa shuti la yadi 25 na kuihakikishia ushindi Argentina na kuingia hatua ya mtoano.
Messi akishangilia baada ya Argentina kuishinda Iran 1-0
22: Ureno yahuwisha matumaini ya kuendelea baada ya kutoka sare ya 2-2 na Marekani katika uwanja wa Manaus. Ronaldo apiga krosi ambayo Silvestre Varela asawazisha katika dakika za lala salama, baada ya kushuhudia bao la Clint Dempsey lingeweza kuizamisha. Ureno yaiombea Ujerumani iifunge Marekani katika mechi ya mwisho, wakati wenyewe wakitakiwa kuichapa Ghana.
Ronaldo akijipumzisha katika dimba la Manaus wakati wa mchezo kati ya Ureno dhidi ya Marekani
25: Messi awa tena mchezaji bora wa mechi na kufunga mara mbili ambapo Argentina inajihakikishia nafasi ya kwanza kwenye Kundi baada ya kushinda 3-2 dhidi ya Nigeria. Alifungua karamu ya mabao dakika ya tatu kasha akafunga kwa shuti la yadi 25 kabla ya mapumziko. Zaidi ya yote, Messi alikuwa na mashuti manne, matatu kati yao yalilenga lango na mawili yaliingia wavuni.
Messi akifunga kwa free-kick, moja kati ya mabao yake mawili katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Nigeria 
Messi akishangilia katika dimba la Porto Alegre baada ya Argentina kusonga hatua ya 16
26: Ronaldo aifungia Ureno bao la ushindi dhidi ya Ghana – lakini haikutosha kuwapeleka hatua ya 16. Matokeo yalikuwa 2-1 lakini walihitaji mabao matatu zaidi kuizuwia Marekani kusonga mbele kwa tofauti ya mabao kufunga na kufungwa. Bao hilo lilikuwa bao la 50 kwa Ronaldo kwa nchi yake na kuwa mchezaji wa kwanza wa Ureno kucheza na kufunga katika fainali tatu za Kombe la Dunia. Pamoja na juhudi binafsi lakini ndoto za kutwaa Kombe la Dunia zilikufa.
Ronaldo akisikitika baada ya Ureno kuondolewa mapema kwenye fainali za Kombe la Dunia licha ya kuifunga Ghana kwenye mchezo wa mwisho hatua ya makundi

JULY
1: Messi tena atajwa mchezaji bora wa mchezo ambapo Argentina yaichapa Switzerland 1-0 shukrani kwa Angel di Maria aliyefunga dakika za lala salama katika muda wa ziada na kutinga hatua ya robo-fainali. Baada ya kupokea mpira kutoka kwa Rodrigo Palacio, Messi aliukokota kabla ya kumpasia Di Maria na kufunga. 
Messi akitafuta mbinu ya kuwatoka mabeki wanne wa Switzerland katika mchezo wao wa 16
5: Katika siku aliyoifikia rekodi ya Diego Maradona ya michezo 91 kwa Argentina, Messi tena atengeneza bao katika mchezo mgumu na kufanikiwa kutinga hatua ya nusu-fainali kwa mara ya kwanza tangu 1990. Messi alitumia akili nyingi ambapo alisaidia kuiua Ubelgiji kwa kuichapa 1-0 shukrani kwa Higuain. Kwa pasi ya Di Maria, Messi alianzisha mashambulizi ambayo yalizaa bao la ushindi. 
Messi akimiliki mpira wakati wa mchezo ambao Argentina iliichapa Ubelgiji bao 1-0 katika dakika nane za mwisho
9: Messi ashtushwa lakini akafunga penalty ya kwanza katika mchezo ulioamuliwa kwa matuta ambapo Argentina iliishinda Uholanzi na kutinga hatua ya fainali. Wanakutana na Ujerumani katika dimba la Maracana baada ya dakika 120 bila kufungana, zinafuatia penalty na Argentina inashinda kwa penalty 4-2.
13: Ilikuwa na maana kuwa wakati wake wa kuvaa taji, lakini Messi hakuweza kuisaidia Argentina kushinda Kombe la Dunia baada ya Ujerumani kushinda taji hilo kwa 1-0 katika mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia kwenye dimba la Maracana. Mchezo huo ulikuwa kama vile Messi vs timu bora duniani lakini hakuweza kutamba. Mario Gotze aliweza, akaifungia Ujerumani bao la ushindi katika dakika ya 113. Juhudi za Messi zikaishia pakavu, lakini aliwahi kupiga adhabuambayo ilitoka kidogo juu ya lango. Messi alifunga mabao manne na kutengeneza moja katika mashindano hayo. Alipata tuzo ya utata ya Golden Ball kwa kuwa mchezaji bora wa mashindano, mbele ya Thomas Muller na Arjen Robben. Rais wa FIFA Sepp Blatter licha ya kueleza mshangao wake kuwa Messi alistahili tuzo, wakati watu waliopo Maradona walisema walichagua mtu siyo. Messi alisema: 'Sijali kuhusu Mpira wa Dhahabu. Nimefadhaishwa na nafasi tulizopoteza. Nilitaka kubeba kombe na kulipeleka Argentina. Maumivu ni makubwa.'
Messi akisikitika baada ya Argentina kuchapwa 1-0 na Ujerumani kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia 
Tuzo ya Mpira wa Dhahabu akipewa mchezaji bora wa mashindano, Messi

AUGUST
12: Alipumzika sana kufuatia Ureno kuondolewa mapema kwenye Kombe la Dunia, Ronaldo arejea kwenye ubora wake na kushinda medali nyingine. Mabao yake mawili dhidi ya Sevilla katika dimba la Cardiff yaifanya Real kushinda UEFA Super Cup na kufanya mpira kuzunguka katika kampeni nyingine ya kufunga na kuvunja rekodi. Baada ya kulikosa akiwa na Manchester United mwaka 2008, mara hii mambo yananyooka na kuongeza mataji katika maktaba ya Ronaldo. Mabao yake mawili yanamuacha Ronaldo akijiunga katika nafasi ya pili kwenye orodha ya wafungaji bora katika mashindano ya Ulaya akiwa na mabao 70.
Ronaldo akihangilia pamoja na James Rodriguez baada ya kufunga dhidi ya Sevilla
19: Ronaldo achezakipindi cha kwanza pekee katika mchezo ambao Real ililazimishwa sare ya 1-1 nyumbani dhidi ya Atletico Madrid katika mchezo wa kwanza wa Super Cup.
22: Mreno acheza kipindi cha pili katika mchezo wa marudiano wa Super Cup lakini ashindwa kuikoa Real baada ya kuchapwa 1-0 na Real kukosa taji lingine.
24: Messi, arejea tena baada ya Kombe la Dunia katika mchezo wa funguzi wa msimu mpya wa La Liga, akifunga mara mbili ambapo Barcelona waliokuwa 10 wakiichapa 3-0.
Messi aanza kampeni yake kwa bao dhidi ya Elche mwezi August 
25: Ronaldo naye aanza harakati zake kuelekea ufungaji bora wa La Liga kwa mara nyingine tena ambapo bao lake la dakika za lala salama laipa Real ushindi wa 2-0 nyumbani dhidi ya Cordoba. Ni mwanzo wa mbio za kufunga mfululizo ambazo zilidumu hadi Novemba.
28: Ronaldo apokea tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Ulaya, kwa msimu wa 2013-14. 
31: Messi amtengenezea Sandro bao la ushindi dhidi ya Villarreal lakini apata majeraha ya musuli katika paja lake la kulia ambapo atakuwa nje ya dimba kwa wiki mbili.

SEPTEMBER
13: Katika Madrid derby ya tatu mwanzo wa msimu, Real yachapwa 2-1 nyumbani na Atletico. Ronaldo alifunga kwa penalty dakika ya 26lakini bao la dakika za lala salama la Arda Turan likaihakikishia ushindi mabingwa watetezi.
16: Real yaanza harakati za kulitetea taji lao la Ulaya kwa ushindi wa 5-1 dhidi ya Basle. Ronaldo afunga bao la tatu katika mchezo walioutawala kwenye dimba la Bernabeu.
20: Real yaichakaza Deportivo La Coruna kwenye dimba la Riazor, huku Ronaldo akiendelea kutamba kwa kufunga hat-trick. Hat-trick hiyo inakuwa ya 20 kwa Ronaldo kwenye La Liga, ikimuweka nyuma ya kinara Telmo Zarra na Di Stefano. Hii ina maana pia kuwa ameifikia rekodi ya Messi ya hat-trick saba ugenini katika ligi.
Ronaldo alifunga hat-trick ambapo Real iliichapa Deportivo 8-2 kwenye dimba la Riazor mwezi Septemba
21: Majeraha yake yamtia wasiwasi, Messi achangia ushindi wa Barcelona wa 5-0 dhidi ya Levante akifunga bao la tatu la msimu.
24: Ronaldo aendelea kufanya mambo baada ya kufunga mara nne katika ushindi wa 5-1 Bernabeu dhidi ya Elche. Mabao mawili yalikuwa ya penalti. Hii ni hat-trick ya 25 kwa Ronaldo katika mashindano yote akiwa na Real Madrid, inamfanya kupitwa tatu nyuma ya panayeshikilia rekodi ya klabu Di Stefano. Afikisha mabao 186 katika mechi 169 za La Liga, Ronaldo aingia katika orodha ya wafungaji bora wa muda wote.
27: Messi na Neymar wafanya mambo makubwa Barcelona ikiigaragaza Granada 6-0 katika dimba la Nou Camp. Neymar afunga hat-trick huku Messi akitupia mara mbili. Mabao hayo yanamfanya Messi kufikisha mabao 400 katika maisha yake ya soka akiwa na umri wa miaka 27. Katika siku hiyo hiyo, Ronaldo aendelea kufunga katika mechi yake ya sitaalipoifungia Real bao la pili dhidi ya Villarreal.
Neymar akifanya mambo yake katika mchezo ambao Barcelonailiichapa Granada 6-0 mwishoni mwa Septemba
30: Messi afunga bao lake la kwanza kwenye Champions League msimu wa 2014-15 lakini walipoteza kwa 3-2 dhidi ya Paris Saint-Germain katika mechi ya pili ya Kundi lao.

OCTOBER
1: Ronaldo asawazisha kwa penalti ambapo Real iliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Ludogorets ya Bulgaria.
4: Messi afunga katika mechi ya tatu mfululizo, alifungua ukurasa wa mabao katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Rayo Vallecano waliokuwa tisa. Ni bao lake la saba la msimu.
5: Ronaldo aendelea kuwa bora katika kuzifumania nyavu, afunga hat-trick nyingine ambapo Real iliisambaratisha Athletic Bilbao 5-0. Ni hat-trick yake ya tatu ya msimu na kufikisha jumala ya mabao 17.
11: Messi aichezea Argentina katika mchezo wa Superclasico dhidi ya Brazil mjini, China. Messi akosa mkwaju wa penalti huku mabao mawili ya Diego Tardelli yakiipa ushindi Brazil.
14: Arejea katika timu ya taifa, Ronaldo afunga kwa kichwa na kuisaidia Ureno kufufua matumaini ya kufuzu Euro 2016 baada ya kuifunga Denmark 1-0. Bao hili linamfanya Ronaldo kuwa miongoni mwa wafungaji bora wa muda wote wa mashindano hayo huku mabao ya kufuzu yakihesabiwa na kuwa na jumla ya mabao 22. Mjini Hong Kong, Messi afunga mara mbili Argentina ikiua 7-0 katika mechi ya kirafiki.
Ronaldo akishangilia bao lake la dakika za lala salama dhidi ya Denmark katika mchezo wa kufuzu Euro 2016
16: Ni miaka 10 leo tangu Messi aanze kuichezea Barcelona.
18: Kwa kufunga Barcelona ikishinda nyumbani 3-0 dhidi ya Eibar, Messi afikisha mabao 250 ya La Liga na kujiweka nyuma ya kinara wa mabao wa ligi hiyo Telmo Zarra. Ronaldo naye aendelea kuzifumania nyavu baada ya kufunga mara mbili Real ikishinda 5-0 dhidi ya Levante; moja kai ya mabao hayo ni penalti.
21: Bao la Messi la dakika ya 24 laisaidia Barcelona kuichapa Ajax 3-1 katika dimba la Nou Camp.
Messi akitoka Kolbeinn Sigthorsson wa Ajax wakati wa mchezo wa Champions League mjini Barcelona
22: Ronaldo afanya mambo Real ikishinda dhidi ya Liverpool 3-0 kwenye dimba la Anfield katika mchezo wa Champions League. Alifunga bao la kwanza dakika ya 23 baada ya kupokea pasi kutoka kwa James Rodriguez. Bao hili lilimaanisha kuwa Ronaldo anakuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika michezo 10 mfululizo ya ugenini kwenye Champions League na kuifikia rekodi ya Messi ya kufunga mabao 22 kwenye mashindano ya Ulaya.
Ronaldo akifunga baada ya kupokea pasi kutoka kwa James Rodriguez kwenye mchezo dhidi ya Liverpool 
Mashabiki kwenye dimba la Anfield wakimzomea winga wa zamani wa Manchester United baada ya kuwafunga
25: Messi na Ronaldo wanakutana kwa mara ya kwanza msimu huu ni ulikuwa usiku mzuri kwa Ronaldo. Baada ya Neymar kufunga bao la kuongoza kwa Barcelona dakika nne baada ya mchezo kuanza, Ronaldo akasawazisha kwa penalti dakika ya 35. Mabao ya kipindi cha pili ya Pepe na Karim Benzema yaliihakikishia Real ushindi wa 3-1. Bao hilo linamfanya Ronaldo kuweka rekodi ya kufikisha mabao 15 katika mechi saba za ligi, akivunja rekodi ya Real Madrid iliyowekwa na Ferenc Puskas, ambaye alifunga mabao 13 katika mechi saba katika misimu yote ya 1959-60 na 1960-1.
28: Wachezaji wote Messi na Ronaldo watajwa kwenye orodha ya wachezaji 23 kuwania tuzo ya FIFA Ballon d'Or 2014. 

NOVEMBER
1: Ronaldo afanya maajabu, afunga mara mbili ndani ya dakika mbili Real ikishinda 4-0 dhidi ya Granada.
5: Usiku wa kihistoria kwa Messi ambapo mabao yake mawili katika ushindi wa Barcelona dhidi ya Ajax mjini Amsterdam unamfanya kuifikia rekodi ya Raul ya ufungaji bora wa muda wote wa Champions League kwa kufikisha mabao 71.
8: Bao la Ronaldo dakika ya 83 laisaidia Real kushinda 5-1 nyumbani dhidi ya Rayo Vallecano.
12: Messi acheza kwenye dimba la West Ham, Upton Park na kufunga penalti katika mchezo ambao Argentina iliichapa Croatia 2-1 kwenye mchezo wa kirafiki. Ni bao lake la 45 katika mechi 96 kwa nchi yake.
Messi akiwa katika dimba linalotumiwa na klabu ya West Ham liitwalo Upton Park wakati wa mchezo wa kirafiki kati ya Argentina dhidi ya Croatia 
14: Ronaldo aendelea kufungulia Ureno njia ya kufuzu Euro 2016 baada ya kuifungia bao katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Armenia.
18: Mahasimu wawili wakutana uso-kwa-uso katika mchezo wa kirafiki ambapo Ureno iliichapa Argentina 1-0 kwenye mchezo uliopigwa Old Trafford mjini Manchester. 
Mahasimu wawili Ronaldo na Messi wakisalimia kabla ya kuanza kwa mchezo wa kirafiki kati ya Ureno na Argentina uliopigwa Old Trafford
22: Messi afunga hat-trick yake ya kwanza ya msimu ambapo Barcelona iliichapa Sevilla 5-1. Lakini ilikuwa bora zaidi pale mabao hayo matatu yakimfanya kufikisha mabao 253 ya La Liga, akivunja rekodi ya Telmo Zarra iliyodumu tangu mwaka 1955. Wakati Uhispania wakishangilia mabao ya Messi, Ronaldo afunga mabao mawili zaidi katika mchezo ambao Real ilishinda 4-0 dhidi ya Eibar.
25: Usiku mwingine wa kihistoria ambapo Messi afunga hat-trick nyingine katika mchezo ambao Barcelona ilishinda 4-0 dhidi ya APOEL mjini Nicosia na kuvunja rekodi ya Raul ya ufungaji bora wa muda wote wa Champions League akifikisha mabao 74.
Messi akishangilia baada ya kuwa mdungaji bora wa muda wote wa Champions League akimpiku Raul
26: Ronaldo afunga bao la 71 kwenye mashindano hayo akifunga bao la ushindi ambapo Real ilishinda 1-0 dhidi ya Basle. Matokeo hayo yanaifanya Real kujihakikishia uongozi wa kundi lao kwa asilimia mia moja.

DECEMBER
1: Kwa mara nyingine tena, Ronaldo na Messi watajwa kuingia tatu bora ya Ballon d'Or. Wanajiunga na mshindi wa Kombe la Dunia Manuel Neuer.
6: Ronaldo afunga hat-trick ya 23 kwenye La Liga na kuwa mchezaji aliyefikisha mabao 200 ya La Liga kwenye historia ya ligi hiyo ambapo Real iliichapa Celta Vigo 3-0.
7: Messi naye yupo katika ubora wake, atupia hat-trick Barcelona ikiichapa Espanyol 5-1 kwenye dimba la Nou Camp.
Messi akiwa na mpira baada ya kufunga hat-trick ambapo Barcelona ilishinda 5-1 dhidi ya Espanyol 
9: Penalti ya Ronaldo dhidi ya Ludogorets inamfanya kufikisha mabao 72 kwenye Champions League, awa nyuma ya hasimu wake mkubwa Messi kwa upachikaji wa mabao.
10: Messi aongeza kasi katika kampeni hiyo baada ya kufunga bao la ufunguzi katika mchezo ambao Barcelona ilishinda 3-1 dhidi ya PSG. Sasa amefikisha mabao 75 ya Champions League.
12: Mabao mawili ya ushindi kwenye La Liga dhidi ya Almeria yanamfanya Ronaldo kufikisha mabao 34 kwa klabu yake na nchi yake.
20: Messi aelekea kufunga mwaka kwa kufunga mara mbili kwenye mchezo ambao Barcelona iliichapa Cordoba 5-0. Afikisha mabao 23 kwenye mashindano yote. Katika siku hiyo hiyo, Ronaldo achangia ushindi wa Real kwa kuifunga mabingwa wa Argentina San Lorenzo kwenye mchezo wa fainali ya Klabu Bingwa Dunia na kutwaa taji hilo nchini Morocco.
21: Ronaldo azindua sanamu lake katika mji wa kwao Funchal, Madeira.  
Ronaldo akiwa na Kombe la Klabu Bingwa Dunia baada ya Madrid kulitwaa nchini Morocco

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.