Online

Sunday, December 20, 2015

Bundesliga: Hannover 96 0-1 Bayern Munich; Bayern yajikita kileleni, Borussia Dortmund yachapwa 2-1 na Cologne, Chicharito afunga bao pekee Bayer Leverkusen ikiichapa Ingolstadt 1-0

Thomas Muller
Bayern Munich itaingia mwaka 2016 ikiwa kileleni mwa msimamo wa Bundesliga kwa pointi nane zaidi baada ya kuichapa Hannover 96 kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa mwisho kabla ya mapumziko ya majira ya baridi.
Mshambuliaji wa Hannover Leon Andreasen na mshambuliaji wa Bayern Robert Lewandowski walikosa mabao kabla ya Thomas Muller kufunga kwa mkwaju wa penalti baada ya Christian Schulz kuushika mpira huku kipa wa Hannover Ron-Robert Zieler akiokoa mabao kadhaa ya Bayern waliotawala mchezo huo.
Kipigo cha Borussia Dortmund cha mabao 2-1 kutoka kwa Cologne kiliifanya Bayern kujikita zaidi kileleni.

Kwingineko kwenye Bundesliga...

Bayern walijikita zaidi kileleni mwa msimamo wa Bundesliga baada ya timu ya nafasi ya pili Borussia Dortmund kuchapwa mabao 2-1 na Cologne.
Bao la ufunguzi la Sokratis Papastathopoulos ilimaanisha kuwa Dortmund imefunga mabao mengi kwenye Bundesliga - 47 - idadi ambayo walifikisha msimu mzima uliopita chini ya Jurgen Klopp. Lakini Simon Zoller na mchezaji wa zamani wa Blackburn anayecheza klabuni hapo kwa mkopo Anthony Modeste waliifungia Cologne.
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Javier Hernandez alifunga bao lake la 10 la ligi katika mechi nane za mwisho Bayer Leverkusen ikiichapa Ingolstadt bao 1-0.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.