Online

Sunday, December 20, 2015

EPL: Chelsea 3-1 Sunderland: Mzimu wa Mourinho waitesa Stanford Brigde

Chelsea
Chelsea wameanza kusahau madhila ya kuanza vibaya kipindi cha Jose Mourinho kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Sunderland katika mchezo wa Premier League uliopigwa Stamford Bridge.
Lakini jambo la kushangaza ni kuwa mashabiki wa The Blues walikuwa na mabango ya meneja wao Mourinho aliyetimuliwa kuzunguka uwanja mzima wa Stamford Bridge wakimsapoti, wakati Diego Costa na Cesc Fabregas wakizomewa kabla na baada ya mchezo wakidaiwa kuwa chanzo cha kufukuzwa meneja huyo.
Branislav Ivanovic aliifungia Chelsea bao la kwanza kwa kichwa huku Black Cats wakiwwekwa kwenye hali mbaya zaidi baada ya Pedro kufunga bao la pili kabla ya mapumziko.
Guus Hiddink, alithibitishwa kuwa mrithi wa Mourinho mpaka mwisho wa msimu, alikuwa jukwaani akiushuhudia mchezo huo sanjari na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba na mmiliki wa klabu Roman Abramovich huku Oscar akifunga bao la tatu kwa penalti baada ya Costel Pantilimon kumchezea vibaya Willian.
Fabio Borini akaifungia Sunderland bao pekee. 
Chelsea
Guus Hiddink, ambaye anachukua mikoba ya Jose Mourinho mpaka mwisho wa msimu, akiangalia mechi sanjari na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba na mmiliki wa timu Roman Abramovich 

Nyota wa Mechi - Oscar (Chelsea)

Oscar
Oscar alikuwa mmoja wa wachezaji muhimu wa Chelsea, akifunga bao moja na alipiga mashuti matano yaliyolenga lango

Dondoo muhimu

  • Branislav Ivanovic alifunga bao lake la kwanza la Premier League akiwa na Chelsea tangu Februari 2015.
  • Chelsea ilifunga mabao mengi kwenye mchezo huu (3)zaidi ya walivyofanya kwenye mechi zao tano za mwisho kwenye Premier League chini ya Jose Mourinho (2).
  • Sunderland imevuna pointi tano kwenye mechi zao 11 za mwisho kwenye Premier League ilizocheza ugenini (W1 D2 L8).
  • The Black Cats imefungwa mabao mengi zaidi (33) na imewaruhusu wapinzani wao kupiga mashuti yaliyolenga lango (106) kwenye Premier League msimu huu.

Kifuatacho?

Chelsea watakipiga na Watford kwenye Boxing Day wakati Sunderland watasafiri kucheza na Manchester City siku hiyo.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.