Online

Sunday, December 20, 2015

EPL: Everton 2-3 Leicester City: Leicester kula Christmas kileleni mwa EPL

Shinji Okazaki and Riyad Mahrez celebrate Leicester's third goal
Leicester City imejihakikishia kuwa kileleni mwa msimamo wa Premier League mpaka christmas baada ya kuichapa Everton mabao 3-2 katika mchezo uliopigwa Goodison Park.
Riyad Mahrez alifunga penalti ya kwanza kati mbili baada ya Ramiro Funes Mori kumvuta jezi Shinji Okazaki.
Romelu Lukaku akasawazisha, lakini kipa wa Everton Tim Howard aliokoa vibaya mpira wa Jamie Vardy na kumruhusu Mahrez kufunga bao la pili.
Okazaki akafunga bao la tatu kwa upande wa Foxes, ambao walimudu kuondoka na pointi tatu licha ya bao la Kevin Mirallas. 

Nyota wa Mchezo - Jamie Vardy (Leicester City)

Jamie Vardy
Kama ilivyokuwa kwa wachezaji-wenza, Vardy alikuwa kila sehemu. Everton walifanya vizuri kumficha ili asifunge, lakini alisaidia mabao mawili

Dondoo unazotakiwa kuzifahamu

  • Ni timu 11 kati ya 23 zilizowahi kuwa kileleni mwa msimamo wa Premier League wakati Christmas ziliishia kutwa taji
  • Jamie Vardy amesababisha penati sita kwenye Premier League tangu mwanzo wa msimu wa 2014-15, nyingi zaidi ya mchezaji yeyote
  • Riyad Mahrez amefunga mabao saba kwenye mechi tisa za Premier League mwezi wa Disemba, ukijuishwa 2015
  • Jamie Vardy amefunga au kutengeneza bao kwenye mechi 15 mfululizo za Premier League, akiimarisha rekodi yake kwenye Premier League
  • Romelu Lukaku ni mchezaji wa kwanza wa Everton kufunga kwenye mechi nane mfululizo kwenye mashindano yote tangu Dave Hickson baina ya Januari na Machi 1954
  • Gareth Barry alicheza mchezo wa 100 wa kimashindano akiwa na Everton; ni timu ya tatu ambayo amewahi angalau kucheza mechi 100 kwenye mashindano yote (pia Man City na Aston Villa)
  • Leighton Baines alianza mchezo wa 250 wa Premier League akiwa na Everton, ni mchezaji wa nne kufanya hivyo baada ya Tim Howard, Leon Osman na David Unsworth

Kifuatacho?

Everton itasafiri kucheza na Newcastle26 Disemba, ikitafuta ushindi wa kwanza baada ya mechi tano, wakati Leicester watawafuata Liverpool, kabla ya kuwakaribisha Manchester City 29 Disemba.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.