Manchester United walijikuta katika hali mbaya dimbani baada ya Norwich kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 kwenye mchezo wa Premier League uliopigwa Old Trafford, huku ikiongeza shinikizo kwa meneja Louis van Gaal.
Licha ya United kumiliki mpira kwa kiwango kikubwa, ilikuwa ni Norwich ambao walipata bao la kuongoza kupitia kwa Cameron Jerome huku United ikizidi kuboronga kipindi cha pili ambapo Jerome alifanya kazi nzuri kisha kumtengea Alex Tettey, ambaye alifunga oa la pili.
Anthony Martial akaifungia United bao la kufutia machozi, lakini United inafikisha mechi ya sita bila ushindi huku Norwich ikiondoka eneo la hatari.

Nyota wa Mechi - Nathan Redmond (Norwich City)

Nathan Redmond
Winga wa Norwich Nathan Redmond alizunguka kila mahala kutafuta mpira

Kifuatacho?

Manchester United watacheza na Stoke kwenye dimba la Britannia 26 Disemba, ikifuatiwa na mchezo dhidi ya Chelsea utakaopigwa Old Trafford siku mbili baadaye.
Norwich wataifuata Tottenham kwenye Boxing Day, kabla ya kucheza na Aston Villa 28 Disemba.

Dondoo unazotakiwa kuzifahamu

  • Alex Neil (miaka 34 na siku 193) ni meneja wa tatu mdogo kupata ushindi wa Premier League ugenini Old Trafford, baada ya Chris Coleman (miaka 33  na siku 137) na Ruud Gullit (miaka 34 na siku 62)
  • Norwich iakuwa timu ya kwanza kupanda daraja na kupata ushindi Old Trafford tangu Bolton mwezi Oktoba 2001
  • Manchester United imefungwa mabao mengi kwenye mechi hii (2) zaidi ya mechi saba za mwisho kucheza nyumbani msimu huu (1)