Online

Sunday, December 20, 2015

Ligue 1: Caen 0-3 Paris St-Germain: Di Maria, Ibrahimovic waipeleka Paris St-Germain kileleni kwa pointi 19, Monaco yabanwa na Troyes

PSG celebrate
Zlatan Ibrahimovic na Angel di Maria walifunga mabao Paris St-Germain ikijikita kileleni mwa msimamo wa Ligue 1 kwa pointi 19 baada ya ushindi wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya Caen.
Di Maria alifungua ukurasa wa mabao kwa shuti la umbali wa yadi 16 kisha Ibrahimovic akishindwa kufunga baada ya shuti lake kuokolewa na Remy Vercoutre.
Lakini akafanikiwa kufunga kabla ya mapumziko kwa shuti la umbali wa yadi 20 na Di Maria akafunga bao lake la sita la ligi tangu alipojiunga na PSG akitokea Manchester United akiunganisha mpira wa kichwa uliopigwa na Lucas Moura.
Zlatan Ibrahimovic
Zlatan Ibrahimovic akifanya mambo yake
Caen walipata penati lakini shuti la Andy Delort liliokolewa na kipa wa PSG Kevin Trapp.
Monaco iliondoa pointi moja kwa PSG kutoka 20 hadi 19 baada ya kulazimishwa sare ya 0-0 dhidi ya Troyes.
Timu ya mkiani Troyes ilipata pointi yao ya nane msimu huu licha ya Mouhamadou Dabo kuoneshwa kadi nyekundu huku Lacina Traore akikosa penalti upande wa Monaco.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.