Online

Sunday, December 20, 2015

Tetesi za usajili: Chelsea na Manchester City zampigania Benzema, Suarez kumfuata Pep Guardiola

Meneja wa Bayern Munich Pep Guardiola ameitaka klabu atakayokwenda kufanya kazi ihakikishe inamsajili fowadi wa Barcelona Luis Suarez, 28, mwenye thamani paundi 100m. (Daily Star)
Aston Villa inataka kuinasa saini ya mshambuliaji wa Gent Laurent Depoitre, 27. (Birmingham Mail)
Chelsea na Manchester City ziko katika vita ya kuwania saini ya fowadi wa Real Madrid Karim Benzema, 28, kufuatia hali ya mambo kalbuni kwake huku akidaiwa kutaka kuondoka Bernabeu mwezi ujao. (Daily Mirror)
Arsenal imeandaa paundi 13.7m kufanya uhamisho wa kiungo wa Inter Milan Marcelo Brozovic, 23. (Metro)
Brentford kuongeza mikataba ya mkopo kwa winga Sergi Canos, 18, na kiungo John Swift, 20, kutoka Liverpool na Chelsea. (getwestlondon.com)
Meneja wa Aston Villa Remi Garde yupo tayari kulipa paundi 6.5m kuinasa saini ya mshambuliaji wa Everton Steven Naismith, 29. (Sunday Telegraph)

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.