Online

Wednesday, December 28, 2016

EPL: Liverpool 4-1 Stoke City: The Reds waipiku Citizen nafasi ya pili EPL

Liverpool ilipunguza pengo la pointi dhidi ya vinara wa Premier League Chelsea hadi kufikia sita na kupaa hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo wakiendeleza rekodi ya kushinda mfululizo nyumbani kufuatia ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Stoke City.
Jon Walters alitangulia kuwafungia wageni kwa kichwa, lakini Liverpool wakasawazisha kupitia kwa Adam Lallana na Roberto Firmino akafunga bao la pili kabla ya mapumziko.
Vijana wa Jurgen Klopp walijihakikishia ushindi, ambao unawafanya wakamate nafasi ya pili kwa pointi moja juu ya timu ya nafasi ya tatu Manchester City - ambao watakutana nao Mwaka Mpya - baada ya Giannelli Imbula kujifunga alipokuwa akijaribu kuokoa krosi ya Divock Origi.
Naye Daniel Sturridge, ambaye alifunga bao lake la kwanza la ligi msimu huu - na bao la 100 kwa Liverpool chini ya meneja Klopp, alifunga bao la nne. 

Sturridge aacha athari

  • Daniel Sturridge alifunga bao lake la kwanza msimu huu, katika jaribio lake la 21 kulitafuta bao
  • Sturridge alifunga sekunde 56 baada ya kuingia uwanjani, bao namba nne la haraka kufungwa na mchezaji wa akiba kwenye Premier League msimu huu
  • Stoke imeruhusu mabao saba kwenye mechi mbili za ugenini zilizopita msimu huu wa Premier League, pungufu bao moja zaidi ya walivyofungwa kwenye mechi zao saba za kwanza ugenini msimu huu (8)
  • Roberto Firmino amefunga mabao mengi ya Premier League mwaka 2016 kuliko mchezaji yeyote wa Liverpool (15)
  • The Reds iliruhusu bao la kwanza kwenye mchezo wa Premier League katika dimba la Anfield kwa mara ya kwanza tangu May (1-1 v Chelsea)
  • Bao la kichwa la Jonathan Walters ambalo lilifungua ukurasa wa mabao lilikuwa bao la 500 msimu huu wa Premier League
  • The Potters imejifunga mabao mengi zaidi kuliko timu yoyote ya Premier League msimu huu (3), yote yakipatikana ugenini

Kifuatacho?

Katika wakati unaoonekana kuwa busy, Liverpool itawaalika Manchester City siku ya Mwaka Mpya kabla ya kucheza na Sunderland saa 46 baadaye. Stoke itasafiri Stamford Bridge siku ya Mwaka Mpya kuwafuata vinara wa ligi Chelsea kisha watawaalika Watford 3 Januari.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.