Online

Tuesday, December 27, 2016

EPL: Premier League round-up: Chelsea yang'ang'ania kileleni, Manchester United, Manchester City na Arsenal zashinda, Leicester City hali mbaya

MECHI 8 za Premier League zimepigwa kwenye Boxing Day, Chelsea ikiindelea kujikita kileleni mwa msimamo huku United, City, Arsenal na Burnley zikitakata. Haya hapa matokeo yote ya mechi zilizopigwa Disemba 27 na dondoo muhimu.

Hull City 0-3 Manchester City

Manchester City imeshinda mechi tatu mfululizo kwenye Premier league kwa mara ya kwanza tangu waliposhinda mara sia mfululizo mwanzoni mwa msimu (ambapo waliminywa Septemba).
Hull imeshinda mara moja katika mechi 16, ikitoka sare tatu na kuchapwa mara 12.
City ilipata clean sheet ya pili kwenye mechi 12 za ugenini.
Yaya Toure amefunga penalti zote 10 za Premier League, rekodi ya 100% kwenye mahindano hayo.Yaya Toure converted a penalty for Man City
Yaya Toure aliifungia Man City kwa penalti
Hull imepigiwa penalti tisa kwenye Premier League msimu huu, nne zaidi ya klabu yoyote (nane kati ya hizo zilifungwa).
Ni Jamie Vardy (10) ameshinda penalti nyingi zaidi kwenye Premier League tangu kuanza kwa msimu wa 2013/14 zaidi ya Raheem Sterling (7).
Hull imeruhusu bao la kwanza mara nyingi zaidi msimu huu kuliko timu yoyote ya Premier League (15).
David Silva (61) ametoa assist nyingi za Premier League kuliko mchezaji yeyote kwenye mashindano hayo tangu alipoanza kucheza ligi hiyo Agosti 2010.
Kelechi Iheanacho amefunga mabao 12 ya Premier League katika mashuti 19 yaliyolenga lango.

Watford 1-1 Crystal Palace

Sam Allardyce ameshindwa kupata ushindi kwenye mchezo wake wa kwanza wa Premier League akiwa meneja katika klabu zake mbili za mwisho (pia Sunderland), baada ya kushinda katika klabu nne (Bolton, Newcastle, Blackburn na West Ham).
Troy Deeney anakuwa mchezaji wa tano kufunga mabao 100 kwenye mashindano yote akiwa na Watford baada ya Luther Blissett, Tommy Barnett, Ross Jenkins na Cliff Holton.
Deeney sasa ni mfungaji wa muda wote wa Watford kwenye historia ya Premier League (mabao 17); moja mbele ya Odion Ighalo (16).Troy Deeney equalised for Watford from the penalty spot
Troy Deeney akiisawazishia Watford kwa penalti
Makipa wote wa Premier League kukutana na penalti 20+, ni David Seaman (32%) ana uwiaono mzuri wa kuokoa zaidi ya Heurelho Gomes (30%).
Christian Benteke amekosa penalti nyingi msimu huu zaidi ya mchezaji yeyote kwenye Premier League (2).
Crystal Palace imeshindwa kuweka clean sheet kwenye mechi 22 kati ya 23 za Premier League (3-0 vs Southampton).
Hii ilikuwa mara ya nne kwenye historia ya Premier League kwamba klabu kuwa wachezaji wawili wa kikosi cha kwanza kutolewa ndani ya dakika 15 za kwanza.
Yohan Cabaye amefunga katika mechi zote za Premier League kwenye dimba la Vicarage Road.

Arsenal 1-0 West Bromwich Albion

Arsenal imefunga kwenye mechi zote 21 za Premier League dhidi ya West Bromwich Albion, rekodi bora ya 100% kwenye mashindano hayo.
Tony Pulis amepoteza mechi zote tisa za Premier League alizotembelea Emirates akiwa meneja, ambapo timu aliyoiongoza imefunga mabao matatu katika mechi hizo.
Mesut Ozil alicheza mchezo wake wa 100 kwenye Premier League, na assist ya 36 kwenye mashindano hayo - ni Eric Cantona pekee ametoa assist nyingi zaidi baada ya mechi 100 (39).
Olivier Giroud amefunga mabao saba katika mechi zake tano za mwisho kwa Arsenal katika mashindano yote.Olivier Giroud headed home the winner for Arsenal
Olivier Giroud aliifungia Arsenal bao pekee
The Gunners waliweka clean sheet kwenye mechi ya tisa ya Premier League, tangu sare ya bila kufungana dhidi ya Middlesbrough Oktoba.
Wakati huo huo, the Baggies imeshindwa kufunga bao kwenye mechi mfululizo kwa mara ya kwanza tangu Septemba.
Arsenal ilikuwa na mashuti 23 zaidi kuliko West Brom (26-3), idadi yao kubwa zaidi kwenye Premier League msimu huu.
Hasa, mashuti 26 ya the Gunners ni mengi zaidi kwao kwenye Premier League tangu walipoichapa Leicester mabao 5-2 Septemba 2015.

Burnley 1-0 Middlesbrough

Burnley ilipata ushindi wao wa kwanza kwenye mechi saba za ligi dhidi ya Middlesbrough (D2 L4).
Middlesbrough imefurahia ushindi mara moja katika mechi 22 za ugenini kwenye Premier League (D6 L15).
Burnley imefunga katika mechi nane kati ya tisa kwenye dimba la Turf Moor.
Middlesbrough haikuwa na shuti lililolenga lango mpaka dakika ya 60, via Gaston Ramirez.Andre Gray scored the decisive goal for Burnley against Boro
Andre Gray akiifungia Burnley bao pekee dhidi ya Boro
Andre Gray alifunga bao lake la kwanza kwenye mechi 10 za 10 za Premier League.
Gray alifunga kwa shuti lake pekee kwenye mchezo.
Sam Vokes amehusika moja kwa moja kwenye mabao sita ya Premier League msimu huu (mabao manne, assist mbili), mawili zaidi ya mchezaji yeyote wa Burnley.
Pointi 19 kati ya 20 za Burnley kwenye Premier League msimu huu zimepatikana katika uwanja wa nyumbani.

Chelsea 3-0 Bournemouth

Chelsea imeshinda mechi 12 mfululizo kwenye ligi kwa mara ya kwanza katika historia yao.
Antonio Conte ni meneja wa kwanza wa Premier League kushinda mechi 15 kati ya 18 za mashindano hayo.
Bournemouth imepoteza mechi tatu kati ya nne za Premier League, ikifungwa mabao matatu katika kila mchezo.
Eden Hazard ni mchezaji wa sita kufunga mabao 50 ya Premier League kwa Chelsea baada ya Frank Lampard, Didier Drogba, Jimmy Floyd Hasselbaink, Gianfranco Zola na Eidur Gudjohnsen.Eden Hazard doubled Chelsea's lead from the penalty spot
Eden Hazard akiifungia Chelsea kwa penalti
Ni Hasselbaink (84), Drogba (106) na Gudjohnsen (153) walifikisha mabao 50 ya Premier League kwa Chelsea katika mechi chache zaidi ya Hazard (155).
Cesc Fabregas ametoa assist 98 za Premier League; ni Wayne Rooney (101), Frank Lampard (102) na Ryan Giggs (162) wametoa assist nyingi zaidi kwenye historia ya mashindano hayo.
Fabregas amefunga au kutoa assist kwenye kila mchezo kati ya michezo mitatu ya mwisho kwenye Premier League aliyoanza kwenye kikosi cha Chelsea (bao moja, assist mbili).

Leicester City 0-2 Everton

The Foxes haijashinda mechi ya Premier League kwenye Boxing Day tangu ilipoichapa Sheffield Wednesday bao 1-0 mwaka 1998 (D1 L6).
Ushindi wa Everton wa mabao 2-0 dhidi ya Leicester ulimaliza mbio za mechi sita za Premier League ugenini bila ushindi.
Joel Robles anakuwa mlinda mlango wa 50 tofauti kutoa assist kwenye historia ya Premier League.
Everton haijafungwa kwenye mechi zao tano za mwisho katika Premier League ilizocheza ugenini kwenye Boxing Day (W3 D2 L0).Romelu Lukaku secured victory for Everton at Leicester
Romelu Lukaku aliifungia Everton dhidi ya Leicester
Romelu Lukaku amefunga mabao saba kati ya mabao 11 ya Everton kwenye mechi za Premier League ilizocheza ugenini msimu huu (64%).
Lukaku amehusika katika mabao 13 kati ya 17 ya Premier League msimu huu (mabao 10, assist tatu).
Kevin Mirallas amefunga katika kila mchezo katika mechi tatu za Premier League dhidi ya Leicester.
Everton imepoteza mara mbili kati ya mechi 14 za Premier League dhidi ya bingwa mtetezi (W7 D5 L2).

Manchester United 3-1 Sunderland

Zlatan Ibrahimovic amehusika katika mabao 14 ya Premier League msimu huu (mabao 12, assist mbili) - angalau mabao manane zaidi ya mchezaji yeyote wa Manchester United.
Fabio Borini alifunga bao lake la kwanza la Premier League tangu May (vs Chelsea).
The Red Devils ilipata ushindi wao wa 19 wa Premier League kwenye Boxing Day, mara nyingi zaidi ya timu yoyote.Henrikh Mkhitaryan scored a superb third for Man Utd
Henrikh Mkhitaryan aliifungia Man U bao la tatu dhidi ya Sunderland
Jose Mourinho ameshinda mara nne kwenye Premier League mfululizo kwa mara ya kwanza tangu Aprili 2015 akiwa na Chelsea.
Assist zote tatu za Paul Pogba kwenye Premier League msimu huu zimemkuta Zlatan Ibrahimovic.
Baada ya kushindwa kufunga kwenye mechi zake 10 za kwanza akiwa na Red Devils kwenye mashindano yote, Henrikh Mkhitaryan amefunga katika kila mchezo katika mechi tatu.
Sunderland imeshinda mara moja katika mechi 25 ilizocheza ugenini dhidi ya Man Utd (D7 L17).
Uwiano wa ushindi wa Jose Mourinho kwenye Premier League akiwa na Man Utd sasa ni 50%, sawa na David Moyes alipokuwa meneja wa Old Trafford.

Swansea City 1-4 West Ham United

West Ham imeshinda mechi tatu mfululizo kwenye Premier League kwa mara ya kwanza tangu Machi.
Swansea imefungwa mabao 29 kwenye ligi tangu Bob Bradley kuchukua mikoba ya umeneja (Okt 15), mengi zaidi ya timu yoyote.
Mabao tisa kati ya 13 ya Andre Ayew kwenye Premier League ameyafungwa katika dimba la Liberty.
Ayew ni mchezaji wa 41 kuifungia na kufunga dhidi ya West Ham kenye Premier League, mengi zaidi ya klabu yoyote.Andy Carroll was on the scoresheet for West Ham at Swansea
Andy Carroll alikuwa mmoja wa wafungaji wa West Ham dhidi ya Swansea
Swansea imeruhusu bao la kwanza kwenye mechi 13 za Premier League msimu huu, ni Hull pekee imeruhusu mabao mengi.
Dimitri Payet ametoa assits 15 za Premier League mwaka 2016, nyingi zaidi ya mchezaji yeyote.
Michail Antonio amefunga mabao 16 ya Premier League kwa West Ham tangu mwanzo wa msimu uliopita, matano zaidi ya mchezaji yeyote.
Mabao yote sita ya Fernando Llorente kwenye Premier League kwa Swansea msimu huu ameyafunga uwanja wa Liberty.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.