Online

Wednesday, December 28, 2016

Tetesi za usajili: Manchester United kula sahani moja na Victor Lindelof, Gibbs kutua Palace, Chelsea kuinasa saini ya Hart, Ben Arfa agomea uhamisho

MENEJA wa Crystal Palace Sam Allardyce anataka kufanya uhamisho wa mlinzi wa pembeni wa Arsenal Kieran Gibbs, 27. (The Sun)
Wakati huo huo, meneja wa Sunderland David Moyes amepanga kuzuwia jaribio la Allardyce kumsajili mshambuliaji Jermain Defoe, 34. (ESPN)
Chelsea imetoa ofa ya paundi 21.3m kwa kiungo wa Atlanta Franck Kessie, 20. (France Football)
Mlinda mlango wa Manchester City Joe Hart, 29, na mwenzie wa Atletico Madrid Jan Oblak, 23, wapo kwenye orodha ya Chelsea kama mbadala wa mlinda mlango wa sasa Thibaut Courtois anayewindwa na Real Madrid. (AS.com in Spanish)
Kiungo wa Paris St-Germain Hatem Ben Arfa, 29, amekataa kuondoka kwa mkopo klabuni hapo kwenda Fenerbahce. (L'Equipe in French)
Windo la Manchester United Victor Lindelof, 22, anataka kusaini mkataba mpya na Benfica ambao utaongeza bei yake kwa zaidi ya paundi 50m. (Daily Mail)
Toulouse imekataa ofa ya paundi 8.5m kutoka West Ham kwa ajili ya mshambuliaji wao Martin Braithwaite, 25. (RMC Sport in French)
Newcastle inavutiwa na mshambuliaji wa Bournemouth Callum Wilson, 24. (The Sun)
Wakati huo huo, the Magpies huenda ikapoteza matumaini ya kumnasa Ruben Loftus-Cheek, 20, ambapo Chelsea imepanga kumtoa kwa mkopo kiungo huyo. (Newcastle Chronicle)
Juventus na Paulo Dybala, 23, hazijafikia muafaka juu ya nyongeza ya mkataba. (Calciomercato.com)
Mshambuliaji wa Cardiff Marouane Chamakh, 32, ameanzisha mazungumzo na klabu ya Al-Arabi ya Qatar. (Mirror)
Klabu ya RB Leipzig ya Ujerumani, nafasi ya pili kwenye msimamo wa Bundesliga, inavutiwa na kiungo wa Leeds United Ronaldo Vieira, 18. (Yorkshire Evening Post)
Ligi Kuu ya Uchina maarufu kama Chinese Super League inataka kumnasa mwamuzi wa Premier League Mark Clattenburg. (Mirror)

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.