Online

Monday, January 23, 2017

Afcon 2017: Burkina Faso 2-0 Guinea-Bissau: Burkina Faso yatangulia robo-fainali

Burkina Faso imefuzu hatua ya robo-fainali ya Africa Cup of Nations wakiwa vinara wa kundi baada ya kuichapa Guinea-Bissau mabao 2-0.
Kujichanganya kwa safu ya ulinzi kuliwapa faida Burkina Faso, baada ya mlinzi Rudinilson Silva kujifunga kwa kichwa mpira ambao ulimzidi mlinda mlango Jonas Mendes.
Fowadi anayekipiga kwa mkopo katika klabu ya Ajax Bertrand Traore akafunga bao la pili baada ya mapumziko.
Cameroon pia ilisonga mbele kama washindi wa pili wa kundi hilo baada ya sare ya 0-0 na wenyeji Gabon ambapo waandaaji hao waliaga mashindano.
Guinea-Bissau, wakicheza kwa mara ya kwanza Africa Cup of Nations, wangaliweza kupata bao la kuongoza, kabla ya Burkina Faso kufanya hivyo.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.