Online

Thursday, January 19, 2017

Afcon 2017: Cameroon 2-1 Guine-Bissau: Simba wasiofungika wapata ushindi wa kwanza Afcon tangu 2010

MABINGWA mara nne wa Afrika Cameroon walipaa kileleni mwa msimamo wa Kundi A wakipigana kutoka nyuma na kuwachapa Guinea-Bissau mabao 2-1 kwenye mchezo wa kundi hilo katika fainali za Mataifa ya Afrika.
Guinea-Bissau, wakicheza kwa mara ya kwanza fainali hizo, walitangulia kufunga kupitia kwa Piquito.
Cameroon wakasawazisha baada ya mapumziko kupitia kwa Sebastien Siani, kisha Michael Ngadeu-Ngadjui akafunga bao la pili na kuipa Cameroon ushindi wa kwanza wa Afcon tangu 2010.
The Indomitable Lions, moja ya nchi yenye historia nzuri katika soka la Afrika, walishindwa kufuzu katika fainali mbili mfululizo zilizopita na walipoteza mechi zote tatu mwaka 2015.
Lakini, baada ya sare ya mchezo wa kwanza dhidi ya Burkina Faso, sasa wana uhakika wa kufuzu hatua ya robo-fainali.
Wanaongoza kundi kwa pointi mbili baada ya mechi tatu za kwanza kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Mapema katika mchezo mwingine wa kundi hilo, waandaaji Gabon walipambana kutoka nyuma baada ya kutanguliwa kwa bao 1-0 na kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang dhidi ya Burkina Faso.
Cameroon itacheza na Gabon wakati Guinea-Bissau watacheza na Burkina Faso kwenye michezo ya mwisho kuamua nani atafuzu robo-fainali kutoka kundi hilo Jumatatu.
Guinea-Bissau italazimika kushinda ili kujiwekea nafasi ya kutinga nane bora.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.