Online

Monday, January 30, 2017

Afcon 2017: DR Congo 1-2 Ghana: Ndugu wawili waipeleka Black Stars kwa Cameroon, Misri yaichapa Morocco

NDUGU wawili wa Ghana Andrew na Jordan Ayew walifunga bao kila mmoja kuisaidia Ghana kuichapa DR Congo mabao 2-1 na kuipeleka Black Stars nusu-fainali ya Africa Cup of Nations.
Fowadi wa Aston Villa Jordan Ayew alikuwa wa kwanza kufunga dakika ya 62, akimtungua mlinda mlango wa TP Mazembe Ley Matampi.
Paul-Jose M'Poku akaisawazishia DR Congo kwa shuti kali nje ya box.
Naye winga wa West Ham Andre Ayew akaihakikishia Ghana ushindi kwa mkwaju wa penalti, akimpoteza Matampi na kuujaza mpira wavuni.
Hiyo inakuwa nusu-fainali ya sita mfululizo kwa Ghana kwenye fainali za Nations Cup, wakikusudia kumaliza ukame wa miaka 35 bila taji la mashindano hayo.
Katika mchezo mwingine wa robo-fainali Misri walikata tiketi ya kucheza nusu-fainali baada ya kuwachapa Morocco bao 1-0.
Kwa matokeo hayo sasa Ghana itacheza na Cameroon katika hatua ya nusu-fainali wakati Misri ikikwaana na Burkina Faso.

Nusu-fainali ya Africa Cup of Nations

  • Burkina Faso v Egypt (Jumatano, 4:00 Usiku)
  • Cameroon v Ghana (Alhamisi 4:00 Usiku)

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.