Online

Thursday, January 26, 2017

Afcon 2017: Misri 1-0 Ghana: Mafarao kukipiga na Morocco tobo-fainali, Ghana v DR Congo Jumapili

Egypt imefuzu hatua ya robo-fainali ya Africa Cup of Nations wakiwa vinara wa Kundi D kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ambayo ilishafuzu Ghana, ambao wanamaliza nafasi ya pili kwenye kundi hilo.
Mohamed Salah alifunga bao pekee katika mchezo huo, akipiga free-kick iliyopita katikati ya ukuta wa walinzi wa Ghana na kujaa wavuni.
Makosa ya mlinda mlango wa Ghana Brimah Razak yalikaribia kumuadhibu lakini kukosa umakini kwa Marwan Mohsen kukainyima Egypt bao la pili.
Daniel Amartey akapoteza nafasi nzuri kwa Ghana, akipiga kichwa fyongo akiunganisha free-kick ya Christian Atsu.
Matokeo hayo yanamaanisha kuwa Egypt watacheza na Morocco wakati Ghana wakipepetana na DR Congo kwenye robo-fainali Jumapili.
Katika mchezo mwingine wa kukamilisha ratiba ya kundi hilo, wawakilishi pekee kutoka Afrika Mashariki Uganda walitoka sare ya bao 1-1 na Mali - sare ambayo hakuna timu iliyonufaika nayo baina yao kwani zote zilishaondolewa.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.