Online

Wednesday, January 25, 2017

Afcon 2017: Togo 1-3 Cong DR: The Leopards watinga robo-fainali, Ivory Coast yalitema kombe

DR Congo imetinga hatua ya nane bora ya Africa Cup of Nations kama vinara wa Kundi C kwa ushindi wa mabao 3-1 ulioiondoa Togo.
Mfungaji kinara wa fainali hizo hadi sasa Junior Kabananga aliunganisha pasi ya Chancel Mbemba kufunga bao la kwanza kwa Congo, likiwa bao lake la tatu katika mechi tatu.
Kabananga akagonga mwamba kwa kichwa kabla ya Ndombe Mubele kufunga bao la pili akimzidi ujanja mlinda mlango wa Togo kufuatia safu mbovu ya ulinzi.
Kodjo Fo-Doh Laba akaifungia Togo bao la kufutua machozi, huku free-kick ya Paul-Jose M'Poku ikaihakikishia DR Congo ushindi.
Katika mchezo mwingine wa kundi hilo, waliokuwa mabingwa watetezi Ivory Coast waliondolewa mashindanoni baada ya kuchapwa bao 1-0 na Morocco, ambao wanafuzu kama washindi wa pili wa kundi.
DR Congo watacheza na mshindi wa pili wa Kundi D kwenye robo-fainali, ambayo inaweza kuwa baina ya Mali, Ghana au - Egypt.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.