Online

Monday, January 16, 2017

Afcon 2017: Tunisia 0-2 Senegal: Sadio Mane aanza shughuli ya mabao AFCON 2017

Senegal ilianza kampeni zake katika fainali za Mataifa ya Afrika kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tunisia katika mchezo wa Kundi B.
Tunisia ilionekana kama ingaliongoza dakika mbili baadaya kuanza mchezo, lakini kichwa cha Ahmed Akaichi kilikosa uelekeo. Na muda mchache baadaye Senegal ikaongoza kupitia mkwaju wa penalti uliopigwa na mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane baada ya Cheikhou Kouyate kuangushwa kwenye box.
Kara Mbodj akafunga bao la pili huku Tunisia wakikosa nafasi kadhaa kupitia kwa Youssef Msakni, ambaye kichwa chake kilikosa uelekeo pia.
Ushindi wa vijana wa Aliou Cisse wanaongoza kundi hilo baada ya Algeria kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Zimbabwe kwenye mchezo wa mwingine wa kundi hilo. Katika mchezo huo, mabao ya Algeria yalifungwa na winga wa Leicester City Riyad Mahrez aliyepachika mabao yote huku mabao ya Zimbabwe yakifungwa na Kudakwashe Mahachi na Nyasha Mushekwi aliyefunga kwa mkwaju wa penalti.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.