Online

Friday, January 6, 2017

African Sports: Riyad Mahrez Mchezaji Bora Afrika

WINGA wa Leicester Riyad Mahrez ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Afrika.
Mahrez, 25, ambaye aliisaidia Leicester City kutwaa taji la Premier League, tayari aliweka kibindoni tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa PFA na tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa BBC.
Fowadi wa Borussia Dortmund na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang alishika nafasi ya pili na mshambuliaji wa Senegal na Liverpool Sadio Mane aliambulia nafasi ya tatu.
Fowadi wa Arsenal na Nigeria Alex Iwobi ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.