Online

Friday, January 13, 2017

Copa del Ray: Barcelona, Real Madrid na Atletico Madrid zatenganishwa Copa del Rey

MABINGWA watetezi Barcelona wamezikwepa Real Madrid na Atletico Madrid baada ya timu hizo bora zaidi katika soka la Uhispania zikitenganishwa kwenye robo-fainali ya Copa del Rey.
Barca itacheza na Real Sociedad, wakati Real Madrid itawaalika Celta Vigo na Atletico Madrid watakutana na Eibar.
Alcoron, timu pekee isiyoshiriki ligi kubaki, imepangwa kucheza na Alaves.
Mechi za kwanza zitapigwa Jumatano na Alhamisi, wakati marudiano yakifanywa wiki moja baadaye.
Barca, ambayo ilipambana kutoka nyuma kwenye mchezo wa kwanza na kuichapa AAthletic Bilbao kwenye hatua ya 16, wana lengo la kuwa timu ya kwanza tangu 1953 kushinda Copa del Rey mara tatu mfululizo.
Droo kamili:
Real Sociedad v Barcelona
Alcorcon v Alaves
Atletico Madrid v Eibar
Real Madrid v Celta

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.