Online

Saturday, January 28, 2017

Copa del Rey: Atletico Madrid kukipiga na Barcelona, Celta Vigo dhidi ya Alaves nusu-fainali Kombe la Mfalme

KLABU za Atletico Madrid na Barcelona zitakutana kwenye nusu-fainali ya Copa del Rey msimu huu.
Mchezo wa kwanza utapigwa katika dimba la Vicente Calderon 1 Februari, huku marudio yakipigwa Nou Camp wiki moja baadaye.
Atletico ilirekodi ushindi jumla wa mabao 5-2 dhidi ya Eibar, wakati Barcelona ikishinda jumla ya mabao 6-2 dhidi ya Real Sociedad.
Droo ya Ijumaa iliwaweka wababe wa Real Mdrid, Celta Vigo dhidi ya Alaves, ambao waliwaondoa Alcorcon.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.