Online

Thursday, January 12, 2017

Copa del Rey: Barcelona 3-1 Athletic Bilbao (4-3 agg): Barca hiyo robo-fainali

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Liverpool Luis Suarez alifunga bao la 100 katika mechi 120 alizoichezea Barcelona miamba hiyo hiyo ya Uhispania  ikitinga robo-fainali ya Copa del Rey kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Athletic Bilbao.
Suarez alifunga bao la kwanza akimalizia krosi ya Neymar katika mchezo uliopigwa Nou Camp na kuifanya Barcelona iwe mbele kwa 1-0 huku wakiwa sare ya mabao 2-2 kutoka katika mchezo wa kwanza.
Suarez anakuwa mchezaji wa tatu kufikisha mabao 100 kwa haraka katika historia ya Barcelona, akitanguliwa na Mariano Martin (mechi 99) na mshambuliaji wa Hungary Laszlo Kubala (mechi 103) wakicheza mechi chache kufikia idadi hiyo. Ilimchukua Lionel Messi kucheza mechi 188 kufikisha mabao 100.
Neymar akafanya matokeo kuwa mabao 3-2 kwa Barcelona baada ya mapumziko akifunga kwa penalti, lakini muda mchache baadaye mshambuliaji wa Athletic Saborit alifunga kwa kichwa na matokeo kuwa mabao 3-3 kabla ya Messi kufunga bao la ushindi kwa Barcelona.
Kichapo kinamaanisha Athletic, ambao wanakamata nafasi ya saba kwenye msimamo wa La Liga, imechapwa na Barca kwenye Copa del Rey kwa misimu mitatu.
Kwingineko kwenye Copa del Alavés ilitoka sare ya bao 1-1 na Deportivo La Coruña ikafanya matokeo jumla kuwa mabao 3-3, lakini Alavés imeshinda kwa mabao ya ugenini. Nayo Córdoba ikachapwa mabao 2-1 na Alcorcón na kufanya matokeo jumla kuwa kama yalivyo na Villarreal ikatoka sare ya bao 1-1 na Real Sociedad huku matokeo jumla yakiwa mabao 4-2 kwa Sociedad.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.