Online

Friday, January 27, 2017

Copa del Rey: Barcelona 5-1 Real Sociedad (6-1): Barca yatinga nusu-fainali ya Copa del Rey kwa mara ya saba mfululizo

MCHEZAJI wa zamani wa Manchester City Denis Suarez alifunga mara mbili mabingwa watetezi Barcelona wakitinga nusu-fainali ya Copa del Rey kwa jumla ya mabao 6-2 dhidi ya Real Sociedad.
Wakiongoza kwa bao 1-0 kutoka kwenye mchezo wa kwanza, Suarez aliongeza uongozi kabla ya Lionel Messi kufunga kwa mkwaju wa penalti.
Juanmi akaifungia Sociedad bao kabla ya Luis Suarez kufanya matokeo jumla kuwa mabao 4-1.
Willian Jose akaifungia Barca bao la nne katika mchezo huo na Suarez akafunga bao la tano likiwa bao lake la pili kwenye mchezo.
Barcelona, ambao wameshinda mashindano hayo kwa historia - mara 28, wanatinga nusu-fainali kwa msimu wa saba mfululizo.
Wanaungana na washindi mara 10 Atletico Madrid, Celta Vigo, ambao waliwaondoa Real Madrid na Alaves kuelekea kwenye droo itakayofanyika Ijumaa.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.