Online

Thursday, January 26, 2017

Copa del Rey: Celta Vigo 2-2 Real Madrid (4-3): Real Madrid yatupwa nje Copa del Rey

Celta Vigo imeidhalili vinara wa La Liga Real Madrid na kutinga nusu-fainali ya Copa del Rey baada ya sare ya mabao 2-2, wakisonga mbele kwa jumla ya mabao 4-3.
Wenyeji walitangulia kufunga kwa bao la mbali baada ya mlinzi Danilo kujifunga.
Cristiano Ronaldo akawasawazishia wageni kwa free-kick, kabla ya Daniel Wass kuirudishia tena Celta uongozi.
Lucas Vazquez akafunga kwa kichwa kwa Real lakini haikutosha.
Zinedine Zidane alishuhudia rekodi yake ya mechi 40 bila kupoteza ikifika kikomo walipochapwa na Sevilla mapema Januari. Sasa wameshinda mara moja pekee katika mechi tano za karibuni kwenye mashindano yote.
"Tulicheza mechi nzuri lakini mwishowe haikuwa rahisi kusonga mbele,''alisema Zidane. "Tumefadhaishwa, lakini tutapambana na kuelekeza nguvu kwenye mashindano tunayoweza kushinda."
Real pia imeshindwa kutinga nusu-fainali ya mashindano haya kwa miaka mitatu sasa, kufuatia kuchapwa na Atletico Madrid kwenye hatua ya 16 mwaka 2015 na kuondolewa mashindanoni kwa kosa la kumchezesha mchezaji asiyestahili mwaka mmoja baadaye.
Kwingineko kwenye Copa del Rey, Atletico Madird walitinga hatua ya nusu-fainali baada ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Eibar, wakisonga mbele kwa jumla ya mabao 5-2, na wanaungana na Alaves baada ya ushindi wao wa mabao 2-0 dhidi ya Alcorcon.
Barcelona, mabingwa watetezi wa mashindano hayo, wanatazamia kutinga nusu-fainali katika mchezo wa pili Alhamisi, watakapocheza na Real Sociedad. Luis Enrique alishinda bao 1-0 kwenye mchezo wa awali.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.