Online

Thursday, January 5, 2017

Copa del Rey: Real Madrid 3-0 Sevilla: James Rodriguez amthibitishia Zidane ana sababu za kuanza kikosi cha kwanza

Real Madrid iliendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo na kufikia mechi 38 baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Sevilla kwenye mchezo wa kwanza wa Copa del Rey hatua ya 16 uliopigwa uwanja wa Bernabeu.
Real - ambayo imeshinda mechi 29 kati ya 38 - iko pungufu kwa mchezo mmoja kuifikia rekodi ya kucheza mechi nyingi bila kupoteza kwenye La Liga.
James Rodriguez alifunga mara mbili akianza kikosi cha kwanza katika mchezo ambao ulimkosa winga Cristiano Ronaldo.
Raphael Varne pia alifunga kwa kichwa na kuiweka Real katika njia nzuri ya kusonga mbele hatua inayofuata watakapokutana tena na Seville kwenye mchezo wa marudiano 12 Januari.
Ni katika mchezo wa marudio ambao unaonesha kuibana zaidi Real ambayo itacheza mara 21 ndani ya wiki 11. 
Madrid ilianza mchezo huo wa nyumbani bila kuwa na nyota wake watatu wa kikosi cha kwanza ambapo Karim Benzema akianzia benchi, Ronaldo alipumzishwa na Gareth Bale atakosekana kutokana na kuugua enka.
Rodriguez aliweka wazi kuwa ataweka mustakabali wake Januari baada ya kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara msimu huu, lakini alianza kikosi cha kwanza akifunga mara mbili bao likiwa na mkwaju wa penalti baada ya Luca Modric kuchezewa faulo na Mariano.
Real Sociedad pia ilijihakikishia nafasi ya kusonga mbele baada ya mabao ya Willian Jose, Carlos Vela na Mikel Oyarzabal kuipa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Villarreal huku Alcorcón ikitoka sare ya 0-0 na Córdoba.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.