Online

Friday, January 13, 2017

Copa del Rey: Sevilla 3-3 Real Madrid (3-6 agg): Real Madrid yaweka rekodi mpya Uhispania

Real Madrid imeweka rekod mpya katika soka la Uhispania ya kutofungwa mechi 40 baada ya bao la Karim Benzema dakika ya 93 kuisaidia timu hiyo kupata sare ya mabao 3-3 dhidi ya Sevilla kwenye mchezo wa pili wa Copa del Rey hatua ya 16.
Mara ya mwisho kwa vijana wa Zinedine Zidane kupoteza mchezo ilikuwa dhidi ya Wolfsburg kwenye robo-fainali ya Champions League Aprili, 2016.
Barcelona ilishikilia rekodi ya awali ya kutofungwa mechi 39, chini ya meneja Luis Enrique baina ya 2015 na 2016.
Sare ya Alhamisi maana yake ni kuwa Real inasonga mbele hatua ya robo-fainali ya Copa del Rey kwa jumla ya mabao 6-3.
Kiungo wa zamani wa Juventus, Real na Ufaransa Zidane, 44, aliteuliwa Januari 2016 baada ya miaka miwili ya kuwa meneja msaidizi.
Ameshinda mataji mengi zaidi ya alivyopoteza mechi - akishinda Champions League, Club World Cup na Uefa Super Cup, wakati alichapwa mechi mbili pekee.
Real imeshinda mara 31 na sare tisa tangu kichapo cha mwisho, ikifunga mabao 115 na kufungwa 39.
Barcelona ilishinda mechi 32 na sare saba katika mashindano yote baina ya Oktoba 2015 na Machi 2016. Walishinda La Liga na kombe msimu huo.
Ikionekana kama Sevilla wanashinda mchezo, Benzema alibadili matokeo ambapo Marcelo aliambaa na mpira mpaka kwenye box na kufunga bao la kusawazisha.
Wenyeji walitangulia kufunga kupitia kwa Danilo ambaye alijifunga, kabla ya shuti la umbali wa yadi 20 la kiungo Marco Asensio kuisawazishia Madrid.
Mabao ya Stevan Jovetic, katika mchezo wake wa kwanza baada ya kujiunga kwa mkopo akitokea Inter Milan, na Vicente Iborra yalimpa Joao Sampoli matumaini ya ushindi.
Lakini Sergio Ramos alifunga kwa penalti na kufanya mabao 3-2 dakika ya 83, huku bao la dakika za lala salama la Benzema likifanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya mabao 3-3.
Kwingineko kwenye Copa del Rey Celta Vigo iliichapa Valencia mabao 2-1 na kufuzu kwa jumla ya mabao 6-2 huku Eibar ikilazimishwa sare ya 0-0 na Osasuna lakini imesonga mbele kwa jumla ya mabao 3-0.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.