Online

Sunday, January 15, 2017

EPL: 2 viwanjani leo EPL: Match Preview: Manchester United v Liverpool: Zlatan Ibrahimovic arejea kuiua Liverpool

MFUNGAJI kinara wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic atachunguzwa, akiukosa mchezo wa nusu-fainali ya kwanza wa EFL Cup dhidi ya Hull kwa sababu ya ugonjwa.
Marcos Rojo pia anweza kurejea, lakini mlinzi-mwenza Eric Bailly yupo kwenye fainali za Africa Cup of Nations.
Winga wa Liverpool Philippe Coutinho anatarajia kucheza mara ya kwanza kwenye ligi tangu Novemba baada ya kuumia enka.
Jordan Henderson na Joel Matip walirejea kwenye mazoezi na wanaweza kucheza, lakini Sadio Mane yupo kwenye Africa Cup of Nations.

Manchester United v Liverpool

Uso-kwa-uso
 • Huu ni mchezo wa 50 wa Premier League baina ya Manchester United na Liverpool - the Red Devils imeshinda mara 27 katika 49 iliyopita (D9 L13).
 • Liverpool imepoteza mara 11 kati ya 14 ya Premier League katika dimba la Old Trafford.
 • Wamepoteza mechi 67 za ligi dhidi ya United, nyingi zaidi ya mpinzani yeyote.
 • Msimu pekee ambao mechi zote mbili zilimalizika kwa sare ya 0-0 ulikuwa 1919-20.
Manchester United
 • United imeshinda mechi tisa zilizopita kwenye mashindano yote, mwendo wao bora tangu mechi 11 Januari-Februari 2009.
 • Wanaweza kushinda mchezo wa saba mfululizo kwenye ligi kwa mara ya kwanza tangu Januari hadi Machi 2013.
 • Kama atacheza, Wayne Rooney atakuwa mchezaji wa 21 wa Premier League kucheza mechi 450 za Premier League.
 • Rooney anahitaji bao moja kuipita rekodi ya Sir Bobby Charlton ya mabao 249 na kuwa mfungaji bora wa muda wote katika historia ya Manchester United.
Liverpool
 • Ushindi utaweka rekodi ya klabu kufikisha pointi 47 baada ya mechi 21 katika msimu wa Premier League, wakiivuka rekodi ya pointi 46 waliyoiweka msimu wa 2008-09.
 • Wameshindwa kufunga bao kwenye mechi mfululizo kwa mara ya kwanza tangu walipocheza mechi tatu bila bao Februari 2016.
 • Liverpool inaweza kusalia bila ushindi kwenye mechi zao nne za kwanza kwenye kalenda ya mwaka kwenye mashindano yote kwa mara ya kwanza tangu 1993.
 • The Reds wamekuwa na clean sheet tatu pekee ugenini kwenye ligi msimu huu.
 • Adam Lallana amehusika katika mabao 14 ya Premier League msimu huu (mabao saba, assist saba), mengi zaidi ya mchezaji yeyote wa Uingereza. 
Mchezo mwingine Jumapili katika Premier League ni baina ya Everton ambao watakuwa nyumbani Goodson Park kuwakaribisha Manchester City.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.