Online

Tuesday, January 3, 2017

EPL: 3 viwanjani leo EPL: Match Preview: Bournemouth v Arsenal: Benik Afobe aikana DRC kuikabili Arsenal

MSHAMBULIAJI Benik Afobe atakuwepo kwenye kikosi cha Bournemouth baada ya kuamua kutoichezea DR Congo katika fainali za Mataifa ya Afrika mwezi huu.
Hata hivyo, mchezaji anayekipiga kwa mkopo Jack Wilshere haruhusiwi kucheza dhidi ya klabu yake na Marc Pugh angali anauguza majeraha yake.
Arsenal inaweza kumkosa kiungo Mesut Ozil, ambaye aliukosa mchezo wa ushindi dhidi ya Crystal Palace kwa sababu ya homa.
Mohamed Elneny yupo kwenye Africa Cup of Nations, wakati Theo Walcott na Kieran Gibbs wanaweza kukosekana kutokana na kuwa majeruhi.

Bournemouth v Arsenal

Uso-kwa-uso
  • Arsenal imeshinda mechi zote tatu za Premier League dhidi ya Bournemouth, ikifunga mabao 10 na kufungwa moja.
Bournemouth
  • Bournemouth imeshinda mechi tano za ligi nyumbani msimu huu, idadi sawa na walivyoshinda katika msimu wa kwanza kwenye Premier League (2015-16).
  • Wamefunga katika mechi zote isipokuwa moja kati ya tisa za ligi ilizocheza nyumbani msimu huu.
  • Hata hivyo, imeruhusu mabao mawili au zaidi kwenye mechi tatu kati ya nne za mwisho ilizocheza Vitality Stadium (W2, L2).
Arsenal
  • Arsenal inaweza kupoteza mchezo wa tatu mfululizo ugenini kwenye ligi kwa mara ya kwanza tangu Agosti - Oktoba 2011.
  • Wamepoteza mechi mbili za mwisho kwenye Premier League ilizocheza ugenini kutoka katika eneo la kushinda.
  • The Gunners imefikisha pointi 40 katikati ya msimu. Walifanya hivi mara moja pekee kwenye misimu sita iliyopita (pointi 42 msimu wa 2013-14).
  • Alexis Sanchez amefunga mabao tisa na kutoa assist tatu kwenye mechi tisa za Premier League ugenini msimu huu.
 Michezo mingine Jumanne hii ni Crystal Palace watakuwa nyumbani Selhurst Park kuwaalika Swansea City wakati Watford watawafuata Stoke City katika dimba la bet365.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.