Online

Saturday, January 21, 2017

EPL: 7 viwanjani leo EPL: Match Preview: Stoke City v Manchester United: Mourinho hafurahia kutokuwa na majeruhi

FOWADI wa Stoke Bojan Krkic atakuwepo tena baada ya kuukosa mchezo wa ushindi dhidi ya Sunderland kwa sababu ya majeraha.
Mame Diouf, Ramadan Sobhi na Wilfried Bony wako katika Africa Cup of Nations lakini meneja Mark Hughes hana tatizo la majeruhi.
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ana kikosi kilicho kamili kuelekea mchezo dhidi ya Stoke.
Mlinzi Eric Bailly atakosekana kwa sababu ya majukumu ya kitaifa akiwa na Ivory Coast kwenye fainali za Mataifa ya Afrika zinazoendelea nchini Gabon.
Mechi nyingi za Premier League Jumamosi ni Liverpool watakuwa nyumbani kuwakaribisha Swansea City wakati Bournemouth wakiwakaribisha Watford. Everton watakuwa wageni wa Crystal Palace wakati West Ham United wakiwafuata Middlesbrough.
West Brom watawaalika Sunderland na Manchester City watakuwa wenyeji wa Tottenham.

Stoke City v Manchester United

Uso-kwa-uso
 • Stoke haijafungwa kwenye mechi tatu za mwisho ilizocheza nyumbani kwenye lingi dhidi ya Manchester United (W2, D1).
 • Bojan Krkic na Marko Arnautovic walifunga kwenye ushindi wa Potters wa mabao 2-0 nyumbani dhidi ya United msimu uliopita.
 • United imeshinda mara moja kati ya nne zilizopita dhidi ya Potters (D2, L1).
Stoke City
 • Stoke imecheza mechi nne za Premier League nyumbani bila kupoteza, ikiwa na clean sheet tatu, na imepoteza mara moja kati ya nane za mwisho ilizocheza bet365 Stadium (W4, D3).
 • Peter Crouch anahitaji bao moja zaidi kuwa mchezaji wa 26 kufunga mabao 100 kwenye Premier League. Kama atafanikiwa Jumamosi atakuwa mchezaji wa kwanza wa Stoke kufunga katika mechi nne mfululizo za Premier League.
 • Mark Hughes amepoteza mara mbili pekee kati ya nane alizocheza nyumbani kwenye ligi akiwa kama meneja dhidi ya Manchester United (W3, D3). Kichapo cha karibuni zaidi ni pale alipochapwa na Manchester City bao 1-0 Novemba 2008.
Manchester United
 • Manchester United haijafungwa kwenye mechi 16 za mashindano yote (W12, D4), huku kichapo cha mwisho wakikipata 3 Novemba ugenini dhidi ya Fenerbahce kwenye Europa League.
 • Wanaweza kushinda mara tano mfululizo ugenini kwenye mashindano yote kwa mara ya kwanza tangu Septemba hadi Oktoba 2012.
 • United haijaruhusu zaidi ya bao moja kwenye mchezo wa Premier League tangu walipochapwa mabao 4-0 ugenini na Chelsea 23 Oktoba.
 • Mabao 14 ya Zlatan Ibrahimovic kwenye ligi yameipa United pointi 11 msimu huu; hakuna mchezaji aliyeipa pointi nyingi timu yake. Diego Costa pia ameipa Chelsea pointi 11.
 • Jose Mourinho amepoteza mara mbili katika mechi tatu za Premier League alizoitembelea Stoke, amepoteza mara nyingi kuliko uwanja mwingine wowote wa Premier League (sawa na uwanja wa Riverside).

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.