Online

Monday, January 2, 2017

EPL: Arsenal 2-0 Crystal Palace: Giroud! Giroud! Giroud!

BAO la mtindo wa nge lililofungwa na Olivier Giroud liliisaidia Arsenal kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Crystal Palace na kuwapeleka hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Premier League.
Akiunganisha krosi ya Alexis Sanchez kutoka nyuma yake, mfaransa Giroud aliunganisha kwa mguu wa kushoto, kisha mpira ukagonga mtambaa panya kabla ya kutua kwenye nyavu nyuma ya mlinda mlango wa Palace.
Naye Alex Iwobi alifunga bao la pili kwa kichwa kuipa Arsenal uhakika wa pointi tatu muhimu kabla ya Palace kumshughulisha mlinda mlango wa Gunners Petr Cech.
Ushindi unawafanya Gunners kuwa nyuma ya vinara Chelsea kwa pointi tisa, wakati Palace wakisalia katika nafasi yao ya 17, pointi mbili juu ya eneo la hatari.
Wageni wameshinda mara moja katika mechi 13 za ligi, huku meneja Sam Allardyce akisubiri kupata ushindi wa kwanza tangu kukabidhiwa timu hiyo kufuatia kutimuliwa Alan Pardew. 
Kwingineko, Harry Kane na Dele Alliwalifunga mabao mawili kila mmoja Tottenham ikibamiza Watford mabao 4-1 na kuingia top four ya Premier League kwa mara ya kwanza tangu Oktoba.

Zawadi ya Olivier - dondoo muhimu

  • Olivier Giroud amefunga mabao manane katika mechi sita alizoanza kwa Arsenal katika mashindano yote.
  • Sam Allardyce hajashinda nyumbani kwa Arsenal akiwa meneja katika mashindano yote, akitoa sare nne na kupoteza mara 12 katika safari zake 16.
  • Tangu kujiunga na klabu, Alexis Sanchez amehusika katika mabao 88 ya Arsenal kwenye mashindano yote (mabao 56, assist 32) - 26 zaidi ya mchezaji yeyote wa Gunners.
  • Arsenal imeshinda mara 130 kati ya mechi 200 za Premier League ilizocheza Emirates chini ya Arsene Wenger (65%) - walishinda 72% ya mechi zao za ligi katika dimba la Highbury chini ya mfaransa huyo (134/186).
  • The Gunners imeweka clean sheet mfululizo katika Premier League iliyocheza nyumbani kwa mara ya kwanza msimu huu, mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa mechi zao tatu za mwisho katika msimu wa 2015-16.
  • Crystal Palace imeshindwa kuwa na clean sheet kwenye mechi 20 za Premier League ilizocheza ugenini, tangu sare ya 0-0 dhidi ya Bournemouth Disemba 2015.
  • Allardyce ameshindwa kupata ushindi katika mechi mbili za kwanza akiwa kama meneja kwenye Premier League kwa mara ya kwanza.

Kifuatacho?

Timu zote zitaingia uwanjani Jumanne. Arsenal itasafiri kuifuata Bournemouth, wakati Palace watawaalika Swansea.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.