Online

Wednesday, January 4, 2017

EPL: Bournemouth 3-3 Arsenal: Olivier Giroud ainusuru Gunners kuangukia pua

Olivier Giroud alikamilisha idadi ya mabao ya kusawazisha katika dimba la Dean Court Arsenal ikitoka nyuma kwa mabao 3-0 na kutoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Bournemouth.
Ilionekana kuwa Arsene Wenger angalikuwa na usiku mbaya baada ya Charlie Daniels kufungua ukurasa wa mabao kwa wenyeji dakika ya 16. Callum Wilson akaifungia bao la pili timu ya Eddie Howe kwa mkwaju wa penalti.
Naye Ryan Fraser akafunga bao la tatu baada ya mapumziko. Lakini Arsenal waliamka ambapo Alexis Sanchez alianza kufungua ukurasa kwa upande wao dakika ya 70 kabla ya Lucas Perez kufunga bao la pili dakika tano baadaye. Arsenal wakanufaika kwa Simon Francis kuoneshwa kadi nyekundu dakika ya 82 na zikaongezwa dakika sita baada ya 90 kukamilika ambapo Olivier Giroud akasawazisha kwa kichwa.
Olivier Giroud akifunga bao la kusawazisha kwa kichwa
Kwingineko, Swansea ilimaliza mbio za mechi nne mfululizo bila ushindi baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace. Angel Rangel alifunga bao la ushindi katika dakika ya mwisho wa mchezo katika mchezo uliopigwa Selhurst Park ambao ulihudhuriwa pia na meneja mpya wa Swansea Paul Clement.
Katika mchezo mwingine, Watford iliendelea kukosa ushindi kwa mchezo wa sita baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Stoke City.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.