Online

Monday, January 23, 2017

EPL: Chelsea 2-0 Hull City: Diego Costa arejea Chelsea ikiongoza msimamo kwa pointi nane

Diego Costa alifunga bao katika kurejea kwake kwenye kikosi cha Chelsea vinara hao wa ligi wakiichapa Hull City mabao 2-0 na kujikita kileleni mwa msimamo wa Premier League kwa pointi nane.
Mshambuliaji wa Uhispania alikosa mchezo wa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya mabingwa watetezi Leicester, akidaiwa kuugua mgongo baada ya kutokubaliana na kocha wa viungo, akidaiwa kutaka kutimkia kwenye Chinese Super League.
Lakini mfungaji huyo kinara wa the Blues - akishangiliwa na mashabiki wa Chelsea - alirejea kwenye kiwango chake cha kufunga dhidi ya Hull, angalifunga kwa shuti la yadi 20 baada ya sekunde 10.
Alifunga bao hilo akimalizia krosi ya winga Victor Moses.
Mchezo huo ulilazimika kuongezwa dakika 7 kipindi cha kwanza baada ya kuumia kwa kiungo wa Hull Ryan Mason, ambaye alilazimika kuwahishwa hospitali baada ya kubebwa kwenye machela kufuatia kukumbana na mlinzi wa Chelsea Gary Cahill.
Hull walicheza vizuri lakini walikosa umakini katika umaliziaji bila majeruhi Robert Snodgrass na Cahill akafunga bao la pili kwa Chelsea akiunganisha kwa kichwa free-kick ya Cesc Fabregas.
Kwingineko kwenye Premier League, Southampton iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya mabingwa watetezi Leicester City katika mchezo uliopigwa mapema kwenye dimba la St Marrys huku Arsenal ikiichapa Burnley mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Emirates.

Dondoo za mechi - Costa afunga bao lililochelewa zaidi kipindi cha kwanza 

  • Ni Ryan Giggs (162) na Frank Lampard (102) wametoa assist nyingi za Premier League zaidi ya Cesc Fabregas (101, sawa na Wayne Rooney).
  • Katika mchezo wake wa 100 akiwa na Chelsea, Diego Costa alifunga bao lake la 52 kwa klabu hiyo.
  • Bao la Costa lilikuwa la kuchelewa zaidi kipindi cha kwanza kwenye Premier League tangu kuanza kurekodiwa kwa muda na Opta (2006-07 - 51:35).
  • Mshambuliaji wa Uhispania amefunga kwenye mechi zote nne za Premier League alizocheza dhidi ya Hull City.
  • Hii ni mara ya nne kwa timu kuwa na pointi 55 au zaidi baada ya mechi 22 za Premier League - na Chelsea sasa imefanya hivyo mara tatu (pia 2004-05 na 2005-06).
  • Hull sasa imecheza mechi 20 za Premier League bila clean sheet tangu walipoichapa Swansea 2-0 Agosti.
  • The Blues sasa imevuna pointi 1,002 za Premier League nyumbani, inakuwa timu ya tatu kufikia tarakimu nne kwenye mashindano hayo (Manchester United 1,116 na Arsenal 1,019).
  • Antonio Conte ana idadi sawa ya pointi katika mechi zake 22 za kwanza kwenye Premier League ambazo Jose Mourinho alikuwa nazo (55).

Kifuatacho?

Chelsea itawaalika majirani zao wa London Brentford kwenye FA Cup raundi ya nne Jumamosi, na itaifuata Liverpool - pointi 10 nyuma yao - kwenye Premier League 31 Januari (20:00).
Hull itawaalika Manchester United kwenye mchezo wa pili wa nusu-fainali ya EFL Cup Alhamisi, wakiwa wamepoteza mchezo wa awali kwa mabao 2-0. Safari ya kuwafuata Fulham kwa ajili ya FA Cup itafuata Jumapili na mchezo ujao wa Premier League watakuwa ugenini dhidi ya United 1 Februari.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.