Online

Monday, January 16, 2017

EPL: Manchester United 1-1 Liverpool: Ibrahimovic aiokoa United OT

BAO la kusawazisha lililofungwa na Ibrahimovic liliipa Manchester United pointi moja baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Liverpool katika mchezo uliopigwa Old Trafford.
Liverpool ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa James Milner dakika ya 27 kwa penalti, aliyozawadiwa baada ya Paul Pogba kuushika mpira katika eneo la box wakati akijaribu kuokoa akichuana na Dejan Lovren.
Mlinda mlango Simon Mignolet alikuwa shujaa wa Liverpool akiokoa hatari kadhaa zilizoelekezwa langoni kwake na Ibrahimovic na Henrikh Mkhitaryan.
Ilionekana kama wageni wanakwenda kushinda na kurejea kwenye nafasi yao ya pili kwenye msimamo wa Premier League, lakini United hatimaye walipata bao la kusawazisha baada ya winga Antonio Valencia kuanza kushangilia baada ya mpira wa kichwa uliopigwa na mchezaji wa akiba Marouane Fellaini kugonga mwamba, kisha akamimina krosi iliyokutana na kichwa cha Ibrahimovic na kusawazisha.
Liverpool sasa wangali katika nafasi ya tatu, pointi saba nyuma ya vinara Chelsea, wakati United - ambayo ushindi mara tisa mfululizo kwenye mashindano yote ulifika mwisho - wako nyuma ya vinara wa ligi kwa pointi 12.
Katika mchezo mwingine wa Premier League uliopigwa mapema Manchester City iliangukia pua baada ya kuchapwa mabao 4-0 na Everton katika mchezo uliopigwa uwanja wa Goodson Park. Mabao ya washindi yalifungwa na Lukaku dakika 34, Mirallas dakika ya 47, Davies dakika 79 na Lookman dakika ya 90'+4.

Milner na bahati yake - dondoo

  • Ni Dwight Yorke na Ruud van Nistelrooy (15) wamefunga mabao mengi kwa Manchester United kwenye mechi zao 20 za kwanza kwenye 20 Premier League zaidi ya Ibrahimovic aliyefunga 14.
  • Liverpool imefunga penalti sita katika dimba la Old Trafford - nyingi katika uwanja wa timu pinzani kwenye Premier League.
  • Milner amefunga penalti yake ya 10 kwenye Premier League, ikijumuishwa saba kwa Liverpool.
  • Mchezaji wa zamani wa England hajapoteza mchezo katika mechi 46 za ligi ambazo alifunga (ushindi mara 37), akiifikia rekodi ya fowadi wa zamani wa Aston Villa Darius Vassell.
  • Wayne Rooney anakuwa mchezaji wa 17 kucheza mechi 450 za Premier League.
  • Boss wa Liverpool Jurgen Klopp amepoteza mara moja pekee katika mechi saba dhidi ya timu pinzani chini ya Jose Mourinho, akishinda tatu.
  • Hii ni mara ya kwanza tangu msimu wa 1987-88 timu hizo kutoka sare katika michezo miwili ya msimu mmoja.

Kifuatacho?

Liverpool itakuwa kwenye FA Cup ambapo itasafiri kuifuata kucheza na timu ya League Two Plymouth Argyle kwa mchezo wa marudiano raundi ya tatu Jumatano. Mhezo wao wa ligi utakuwa nyumbani dhidi ya Swansea Jumamosi, ambapo Manchester United itaitembelea Stoke City siku hiyo.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.