Online

Monday, January 2, 2017

EPL News: Bao la Olivier Giroud ni moja ya mabao bora matano kwa Arsenal - Arsene Wenger

BAO la style ya nge lililofungwa na mshambuliaji Olivier Giroud kwenye ushindi wa Arsenal wa mabao 2-0 dhidi ya Crystal Palace ni moja kati ya "mabao matano bora" ya meneja Arsene Wenger katika kipindi cha miaka 21.
Mabao ya Thierry Henry na Dennis Bergkamp ni miongoni mwa mabao bora ya Wenger lakini alisema "hili litakuwa bao la Giroud".
Aliongeza: "Kiufundi haiwezekani lakini unatakiwa kuwa nalo. Krosi haikuja kimawazo na Olivier alifanya kitu fulani maalum."
Fowadi wa Ufaransa Giroud alisema bao lake "lina bahati sana".
Mbinu ya ushambuliaji wa kushtukiza iliishia kwa Giroud kuuganisha krosi ya Alexis Sanchez kutoka nyuma yake ikapitia juu ya bega kabla ya mpira kuishia langoni, ukigonga mwamba.
Bao hilo lilifungua mlango Arsenal ikitinga nafasi ya tatu.

Mabao bora ya Wenger kwa miaka 21 ya kuwa meneja wa Arsenal

Leicester 3-3 Arsenal, 27 Agosti 1997
Mshambuliaji wa Uholanzi Dennis Bergkamp alionesha utaalamu wake wa kucheza na mpira akiuzungusha mpira hewani kwa mguu wa kushoto, kisha akamzunguka Matt Elliott upande wa kulia, kisha akaupiga mpira langoni akimzidi ujanja mlinda mlango Kasey Keller.

Newcastle 0-2 Arsenal, 3 Machi 2002
Huenda ni bao maarufu zaidi la Bergkamp katika mabao yake 120 akiwa na Arsenal lilikuja dhidi ya Newcastle, ambapo aliuwahi mpira kumzunguka Nikos Dabizas kwa mguu wake wa kushoto, kabla ya kumtungua mlinda mlango Shay Given kwa mguu wa kulia.

Real Madrid 0-1 Arsenal, 21 Februari 2006
Henry alifanya mambo ya ajabu kwa kufunga mabao mazuri wakati wa muda wake katika kikosi cha Arsenal, lakini bao lake la ushindi dhidi ya Real Madrid katika dimba la Bernabeu mwaka 2006 ni bao la kwanza linalompendeza Wenger.
Mshambuliaji huyo wa Ufaransa aliunasa mpira katikati ya uwanja, akageuka, akakimbia nao akiwapita walinzi watatu, akimchambua kila mmoja, akafunga kwa mguu wa kushoto.

Arsenal 4-2 Liverpool, 4 Aprili 2004
Miama miwili nyuma, Henry alifanya kama kile alichokifanya dhidi ya Madrid.
Aliupokea mpira katikati ya uwanja huku walinzi wa Liverpool wakiwa mbele yake, mfaransa huyo akacheza na kuwapita walinzi kabla ya kuufungua mwili wake na kuachia mkwaju mkali uliomzidi kipa wa Liverpool Jerzy Dudek.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.