Online

Thursday, January 12, 2017

EPL News: Dimitri Payet hataki kuichezea West Ham - Slaven Bilic

MENEJA wa West Ham United Slaven Bilic anasema fowadi Dimitri Payet hataki tena kuichezea klabu hiyo - lakini hawatomuuza.
Payet, 29, amekuwa akihusishwa mara nyingi na kutaka kuihama timu hiyo.
"Tumeshasema hatuuzi wachezaji wetu bora lakini Payet hataki kucheza kwetus," alisema Bilic. "Hatutomuuza."
Payet alijiunga West Ham akitokea Marseille kwa paundi 10.7m June 2015. Msimu wake wa kwanza ulikuwa mzuri, akifunga mabao 12 na akatajwa kuwania tuzo ya PFA.
Mwezi Februari 2016 alisaini mkataba mpya ambao utamfanya kuitumikia Hammers hadi majira ya joto 2021.
Hata hivyo, licha ya kufunga mara tano msimu huu, Payet ameshindwa kuwa na kiwango kizuri msimu huu, na gazeti la the Sun liliarifu wiki iliyopita kuwa Bilic amemuagiza mchezaji huyo kuimarisha mwenendo wake.
"Nataraji kutoka kwake kurejea na kuonesha ushirikiano kwa timu kama timu inavyomuonesha," alisema Bilic Ijumaa iliyopita.
"Hatutomuuza, kwa namna yoyote. Siyo tatizo la fedha au chochote. Tunawataka wachezaji wetu bora.
"Nilizungumza na mwenyekiti na hii siyo sababu ya fedha. Tulimpa mkataba mrefu kwa sababu tunamhitaji."
Aliwekwa nje kwenye mchezo wa Ijumaa ambao walichapwa mabao 5-0 na Manchester City kwenye FA Cup.
"Amekuwa akiwindwa na baadhi ya klabu au vyovyote," aliongeza Bilic. "Hiyo ni kawaida katika kipindi hiki cha mwaka.
"Lakini mpaka atakapobadilisha tabia yake yupo nje ya timu na hatofanya mazoezi na sisi."
West Ham inakamata nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Premier League, pointi saba kutoka eneo la kutelemka daraja, na itaialika Crystal Palace Jumamosi.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.