Online

Monday, January 30, 2017

EPL News: Jose Mourinho amfungulia milango Ashley Young kuondoka Manchester United

MENEJA wa Manchester United Jose Mourinho amedai kuwa winga Ashley Young anaweza kuondoka klabuni hapo siku ya mwisho wa dirisha la usajili.
Young, 31, ambaye ameanza mara mbili pekee kwenye kikosi cha kwanza katika Premier League, amekuwa akihusishwa na kutaka kutimkia klabu za Everton, Swansea City, Crystal Palace na Watford.
Mourinho alibainisha kuwa Young ni mchezaji pekee wa United ambaye anaweza kuondoka kabla dirisha la usajili halijafungwa Jumanne usiku, lakini akasisitiza anamtaka mchezaji huyo kubaki Old Trafford.
‘Mchezaji pekee ambaye nina uhakika wa kuondoka – na nasubiri hadi Januari 31 kujua kitu kinachoendelea – ni Ashley Young,’ alisema Mourinho.MANCHESTER, ENGLAND - SEPTEMBER 24: Wayne Rooney of Manchester United (L) shares a smile with Ashley Young of Manchester United (R) while sitting on the bench  during the Premier League match between Manchester United and Leicester City at Old Trafford on September 24, 2016 in Manchester, England.  (Photo by Clive Brunskill/Getty Images)
Young amecheza mara 10 pekee kwenye kikosi cha United msimu huu. (Getty Images)
‘Mchezaji ambaye ningependa kumbakisha.
‘Sifurahii kama ataondoka lakini ni mchezaji pekee ambaye nilithibitisha anaweza kuondoka, ndiyo maana sikumchezesha, ndiyo maana natoa nafasi kwa watu wengine kwa sababu sijui kama atabaki nasi.
‘Kama ningechagua, ndiyo hasa, atabaki nasi.’

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.