Online

Monday, January 30, 2017

EPL News: Ni Arsenal na Tottenham pekee zinaweza kuizidi Chelsea - Rio Ferdinand

MLINZI wa zamani wa Manchester United na England Rio Ferdinand anaamini kuwa ni Arsenal na Tottenham pekee ndizo zinazoweza kuizidi Chelsea katika mbio za ubingwa msimu huu.
Vijana wa Antonio Conte wanaongoza msimamo wa Premier League kwa pointi nane, huku Arsenal katika nafasi ya pili na Tottenham, ambayo iko nyuma ya Chelsea kwa pointi tisa, inakamata nafasi ya tatu.
Ferdinand anaamini kuwa Liverpool itaondolewa kwenye mbio za ubingwa kama watashindwa kuichapa Chelsea kwenye mchezo wa Premier League utakaopigwa Anfield Jumanne usiku.
‘Zipo njia za kuifikia Chelsea. Kuna uwazi nyuma ya mawinga wa nyuma. Lakini wanajua namna ya kupata matokeo Anfield,’ Ferdinand aliandika katika makala yake iliyochapishwa na The Sunday Times.LIVERPOOL, ENGLAND - JANUARY 28: Jurgen Klopp the head coach / manager of Liverpool during The Emirates FA Cup Fourth Round between Liverpool and Wolverhampton Wanderers at Anfield on January 28, 2017 in Liverpool, England. (Photo by Matthew Ashton - AMA/Getty Images)
Ferdinand anaamini Liverpool itaondolewa kwenye mbio za ubingwa kama hawatoifunga Chelsea. (AMA/Getty Images)
LONDON, ENGLAND - JANUARY 22: Diego Costa (R) of Chelsea celebrates scoring the opening goal with his team mates during the Premier League match between Chelsea and Hull City at Stamford Bridge on January 22, 2017 in London, England. (Photo by Richard Heathcote/Getty Images)
Chelsea inaongoza msimamo wa Premier League kwa pointi nane. (Getty Images)
‘Kama Liverpool hawatoshinda, watakuwa nje ya mbio za ubingwa – ingawa kiuhalisia naziona Arsenal na Tottenham kama klabu pekee zinazoweza kuishinda Chelsea.
‘Liverpool, Manchester United na Manchester City zinapambana tu chini yao. Mbio za ubingwa zimebaki London. Nafasi ya nne inapiganiwa na Kaskazini-magharibi.’

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.