Online

Friday, January 13, 2017

EPL News: Nyota wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic atwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Premier League mwezi Disemba

MSHAMBULIAJI wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic ametajwa kuwa Mchezaji Bora wa Premier League mwezi Disemba.
Zlatan aliwazidi Alexis Sanchez, Diego Costa na Dele Alli kushinda tuzo hiyo kwa mara ya kwanza.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Ajax, 35, alifunga mabao matano katika mechi sita katika mwezi ambao vijana wa Jose Mourinho hawakupoteza mchezo.
Hiyo ni baada ya kusota Oktoba na Novemeba ambapo alifunga bao moja katika michezo 11 lakini alirejea kwenye kiwango chake huku Manchester United ikiiwinda nafasi katika top four.
Vijana wa Mourinho watacheza Liverpool Jumamosi katika dimba la Old Trafford na Ibrahimovic anatarajia kuanza baada ya kuukosa mchezo wa EFL Cup Jumanne dhidi ya Hull kutokana na kuumwa.
Ibrahimovic ana mabao 18 katika mechi 28 msimu huu.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.