Online

Thursday, January 12, 2017

EPL News: Olivier Giroud, Laurent Koscielny na Francis Coquelin yawanogea Gunners

WACHEZAJI watatu wa Arsenal Olivier Giroud, Laurent Koscielny na Francis Coquelin wamesaini nyongeza ya mkataba wa kuitumikia klabu hiyo.
The Gunners haikubainisha muda wa nyongeza katika dili hilo la mshambuliaji Giroud, 30, mlinzi Koscielny, 31, na kiungo Coquelin, 25.
Lakini Koscielny alisema kwenye Twitter angaliongeza "safari yake ... mpaka 2020".
"Tunafurahi sana kuwa wachezaji wetu muhimu watatu wamekubali kukaa nasi kwa muda mrefu," alisema boss wa Gunners Arsene Wenger.
Watatu kutoka timu ya Taifa la Ufaransa wanakuwa wachezaji wanaocheza mara kwa mara katika kikosi cha Arsenal, ambapo Giroud alisaini dili mpya akiwa na mabao manne katika mechi nne - likiwemo bao la 'scorpion' dhidi ya Crystal Palace.
"Francis amekuwa mwenpesi wa kujifunza katika miaka michache iliyopita kwa sababu anazingatia kila siku," alisema Wenger.
"Olivier ana uzoefu mkubwa kwenye mechi sasa na amekuwa mchezaji mwenye ushindani zaidi tangu alipojiunga nasi.
"Laurent ni sababu sehemu muhimu kwenye kikosi chetu na naamini mmoja kati walinzi bora zaidi dunia kwa sasa. Kwa jumla, hii ni taarifa njema kwetu."

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.