Online

Sunday, January 15, 2017

EPL: Premier League round up: Chelsea yasogea na saba zaidi kileleni, Spurs, Arsenal zaiengua Liverpool

Chelsea ilipaa kileleni mwa msimamo wa Premier League kwa pointi saba baada ya kazi nzuri bila uwepo wa Diego Costa wakishinda mabao 3-0 dhidi ya Leicester.
Mabao mawili ya Marcos Alonso yaliisaidia vinara hao kuisambaratisha Leicester ambayo haikuwa na nidhamu ya ulinzi.
Pedro akaongeza bao la tatu katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la King Power baada ya kupoteza katika mchezo ambao uligharimu kibarua cha boss wa zamani Jose Mourinho msimu uliopita.

Tottenham 4-0 West Brom
Harry Kane alifunga hat-trick Tottenham ikiichapa West Brom mabao 4-0 na kukaa nafasi ya pili kwenye msimamo wa Premier League.
Liverpool na Manchester City zitakuwa uwanjani Jumapili, Spurs waliongeza shinikizo kwa vinara Chelsea walipokuwa na kiwango bora katika dimba la White Hart Lane.
Kane, ambaye alikosa mchezo wa FA Cup dhidi ya Aston Villa baada ya kuzaliwa kwa mtoto wake wa kwanza, alifungua karamu ya mabao dakika ya 12, kabla ya bao la kujifunga la Gareth McAuley kufanya matokeo kuwa mabao 2-0.
Kane akafunga bao lingine akimalizia krosi ya Kyle Walker na kukamilisha hat-trick zikisalia dakika nane.
Unakuwa ushindi wa sita mfululizo kwa Spurs kwenye Premier League, ambao unawaweka pointi moja juu ya the Reds na saba nyuma ya Chelsea, wakati West Brom walichapwa mara ya kwanza katika dimba la White Hart Lane tangu 2012.

Swansea City 0-4 Arsenal
Arsenal ilipanda hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo, juu ya Liverpool kwa tofauti ya mabao, baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Swansea wakimfanya boss wa Swans Paul Clement akipoteza mchezo wa kwanza nyumbani na kuifanya timu hiyo kukaa mkiani.
Olivier Giroud alianza kufunga dakika saba kabla ya mapumziko na The Gunners wakapata bao la pili dakika ya 56 baada ya krosi ya Alex Iwobi kuita juu ya kiungo wa Swansea Jack Cork.
Dakika 10 baadaye, mlinzi Kyle Naughton alijifunga, na Alexis Sanchez akafunga bao la nne zikisalia dakika 18.

Watford 0-0 Middlesbrough
Uwanja wa Vicarage Road ulijawa na huzuni kubwa baada ya mashabiki kuomboleza kifo cha meneja wa zamani wa Watford Graham Taylor, ambaye aliaga dunia Alhamisi kufuatia maradhi ya moyo, kuelekea mchezo wake dhidi ya Middlesbrough.
Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 0-0.
Meneja mpya wa Hull Marco Silva alipata ushindi wa kwanza kwenye Premier League akishinda mabao 3-1 dhidi ya Bournemouth katika mchezo uliopigwa KCOM.
The Cherries walitangulia mbele dakika ya tatu kupitia kwa Junior Stanislas aliyefunga kwa mkwaju wa penalti.
Abel Hernandez akafunga kwa kichwa kusawazisha na kisha shuti la Tom Huddlestone likambabatiza Tyrone Mings the Tigers wakiibuka na ushindi.

Sunderland 1-3 Stoke City
Stoke iliongeza presha kwa Sunderland bada ya kuichapa mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa Stadium of Light.
Marko Arnautovic alifungua ukurasa wa mabao dakika ya 15 kisha akafunga bao la pili kwa Stoke.
Peter Crouch akafunga bao la tatu dakika ya 35 na, licha ya Jermain Defoe kufunga, hapakuwa na njia kwa David Moyes kuepa kichapo.

West Ham 3-0 Crystal Palace
West Ham ilisahau mambo ya Dimitri Payet na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Crystal Palace katika mchezo uliopigwa London Stadium.
Sofiane Feghouli aliifungia Hammers bao la kuongoza dakika ya 66, kabla ya Andy Carroll kufunga bao la pili zikisalia dakika 12 na Manuel Lanzini akafunga bao la tatu.

Burnley 1-0 Southampton
Burnley iliendelea kuimarika baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Southampton baada ya Joey Barton kufunga bao pekee dakika ya 79 kwa free-kick.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.