Online

Tuesday, January 3, 2017

EPL: Premier League round-up: Manchester United yashinda tena, Liverpool yampa zawadi ya penalti Defoe, West Brom, Everton zashinda

LIGI Kuu ya England iliendelea Jumatatu kwa mechi sita kupigwa katika viwanja sita tofauti. Manchester United yaendelea kushinda, Liverpool yabanwa huku mabingwa watetezi Leicester City wakizidi kupotea katika ramani ya kutetea ubingwa wao. Hizi hapa dondoo muhimu sana kuzifahamu baada ya mechi za Premier League zilizopigwa Jumatatu, kwa msaada wa Opta...

Middlesbrough 0-0 Leicester City 

Leicester imevuna pointi 21 kutoka katika mechi 20 za awali kwenye PL, ni chache sana kuwahi kukusanywa na mabingwa watetezi wa Premier League.
Middlesbrough haijashinda kwenye mechi zao 14 za ligi zilizopita dhidi ya Leicester (D8 L6), tangu ushindi wa bao 1-0 katika dimba la Riverside Machi 2002.
Hasa, michezo 14 ya Middlesbrough bila ushindi dhidi ya Leicester ni nyingin mno kwa sasa kuliko dhidi ya timu yoyote.Marten de Roon runs at the Leicester City defence
Marten de Roon akiichambua safu ya ulinzi wa Leicester City
Jumla ya pointi tatu za Leicester kwenye mechi 10 za kwanza ugenini msimu huu ni chache sana kuwahi kupata bingwa mtetezi.
The Foxes haijashinda kwenye mechi zao 12 za Premier League ilizocheza ugenini, ikitoka sare tano na kupoteza saba.
Wes Morgan amecheza kila mchezo kati ya michezo 81 iliyopita ya Leicester kwenye Premier League, ni nyingi sana kuliko mchezaji yeyote wa ligi hiyo kwa wakati huu.
Hii ni mara ya tatu kwa Leicester kushindwa kufunga kwenye mchezo wa ugenini kwenye Premier League tangu kuanza kwa mwaka 2016.
Brad Guzan aliweka clean sheet mfululizo kwenye Premier League kwa mara ya kwanza tangu Januari 2015.

Everton 3-0 Southampton 

Everton haijafungwa kwenye mechi zao 12 zilizopita kwenye Premier League ilizocheza nyumbani dhidi ya Southampton (W9 D3), ikifungwa mabao sita pekee.
Bao la Enner Valencia lilikuwa bao lake la kwanza kwenye Premier League tangu Januari 2016 (alipofunga mara mbili dhidi ya Man City akiwa West Ham).
Leighton Baines anakuwa mlinzi wa tatu kufunga mabao 30 ya Premier League baada ya John Terry (40) na David Unsworth (38).Enner Valencia celebrates after opening the scoring for Everton against Southampton
Enner Valencia akishangilia baada ya kufungua ukurasa wa mabao kwa Everton dhidi ya Southampton
The Toffees imefunga angalau mabao mawili kwenye mechi tano kati ya sita za Premier League, ikishindwa kufunga kwenye mechi moja (0-1 vs Liverpool).
Southampton imepoteza mechi tatu mfululizo kwenye Premier League kwa mara ya kwanza tangu Disemba 2014 (mechi nne).
Romelu Lukaku amehusika katika mabao 15 ya Premier League msimu huu (mabao 11, assist 4) - angalau mabao 10 zaidi ya mchezaji yeyote wa Everton.
Tangu alipoanza kuichezea Everton mwezi Septemba 2013, ni Sergio Aguero (77) na Harry Kane (59) wamefunga zaidi kwenye Premier League kuliko Lukaku (54).
Ronald Koeman anakuwa meneja wa kwanza kuwachezesha makinda wawili kwenye mchezo wa Premier League (Calvert-Lewin na Davies) tangu Louis van Gaal akiwa na Manchester United dhidi ya Bournemouth May (Borthwick-Jackson na Rashford).

Manchester City 2-1 Burnley 

Sergio Aguero alifunga akitokea kwenye benchi kwa mara ya kwanza kwenye Premier League tangu Agosti 2014 v Liverpool.
Raheem Sterling amehusika moja kwa moja kwenye mabao tisa ya Premier League kwa Man City msimu huu (mabao 5, assist 4), ukilinganisha na mabao manane ya msimu wake wa kwanza akiwa na klabu hiyo.
Fernandinho ameoneshwa kadi nyekundu mara tatu katika mechi zake sita akiwa na Manchester City katika mashindano yote.
Ni mchezaji wa kwanza wa City kuoneshwa kadi mbili nyekundu kwenye msimu wa PL tangu Mario Balotelli msimu wa 2011/12.Sergio Aguero scored Man City's decisive second
Sergio Aguero aliifungia Man City bao la pili
Gael Clichy alifunga bao lake la tatu kwenye Premier League baada ya mechi 311 (2 kwa Man City, 1 akiwa Arsenal). Bao lake la mwisho alilifunga Novemba 2014 v Southampton.
Man City imeweka clean sheet kwenye mechi mbili kati ya 10 za Premier League ilizocheza Etihad msimu huu.
Bao la Burnley lilikuwa la tatu kulipata ugenini msimu huu.
The Clarets imevuna pointi moja katika mechi zake za ugenini msimu huu, huku pointi 22 kati ya pointi zake 23 wakizipata Turf Moor (D1 L8 ugenini).

Sunderland 2-2 Liverpool 

Kufuatia sare ya Jumatatu, Liverpool imepoteza mchezo mmoja kati ya 18 ya Premier League (W12 D5).
David Moyes ameshinda mara moja katika mechi zake 17 za Premier League akiwa kama meneja dhidi ya Liverpool (D6 L10)
Jack Rodwell alianza kwa mara ya 34 kwa Sunderland lakini bado hajashinda (D16 L18); akiendeleza rekodi ya Premier League.
Jermain Defoe anakuwa mchezaji wa nne kufunga mabao 10+ kwenye misimu 10 tofauti ya Premier League sambamba na Alan Shearer, Wayne Rooney na Frank Lampard.Jermain Defoe scored two penalties against Liverpool
Jermain Defoe alifunga penalti mbili dhidi ya Liverpool
Defoe amefunga mabao 11 katika mechi 19 za Sunderland kwenye Premier League msimu huu.
Sunderland ni timu ya kwanza kufunga penalti mbili kwenye mechi moja ya Premier League dhidi ya Liverpool tangu West Brom Aprili 2011.
Daniel Sturridge amefunga mfululizo kwenye mechi za Premier League baada ya kucheza mechi 12 bila bao.
Sadio Mané amehusika katika mabao matano kwenye mechi saba za Premier League (mabao matatu, assist mbili).
Mané amefunga katika mechi mbili kati ya tatu za Premier League alizocheza Stadium of Light.

West Bromwich Albion 3-1 Hull City 

West Brom imefunga mabao 3+ katika mechi tano tofauti za nyumbani kwenye ligi msimu huu, mengi zaidi ya msimu wowote uliopita wa Premier League.
Hull imecheza mechi 22 katika mashindano yote bila clean sheet, rekodi yao mbaya sana (pia mwaka 1936 na 1991).
The Tigers imepoteza kila mchezo kati ya michezo minane ya Premier League iliyocheza ugenini, rekodi mbaya sana tangu Newcastle ilipopoteza mechi tisa mfululizo Aprili 2016.
Robert Snodgrass amehusika moja kwa moja katika mabao tisa kati ya 17 ya Hull kwenye Premier League msimu huu (mabao 7, assist 2).Chris Brunt got West Brom back on course
Chris Brunt aliirejesha West Brom kwenye mstari
Ahmed Elmohamady alitoa assist kwa mara ya kwanza katika mechi zake 22 za Premier League (tangu May 4 2015).
Matt Phillips amehusika moja kwa moja kwenye mabao 12 katika mechi 19 msimu huu (mabao 4, assist 8), yakiwepo manne katika mechi mbili (bao 1, assist 3).
Kwa bao la Brunt, the Baggies wanakuwa timu ya kwanza kufikia idadi mara mbili ya mabao ya kichwa kwenye Premier League msimu huu (10, kufikia 11 via bao la McAuley).
Hii ni mara ya pili pekee wachezaji wawili wa Ireland Kaskazini kuifungia timu kwenye mchezo mmoja wa Premier League (pia Brunt & Jonny Evans kwa West Brom v Watford Disemba 2016).

West Ham 0-2 Man Utd 

Manchester United sasa imecheza mechi 13 bila kufungwa katika mashindano yote; rekodi yao nzuri tangu Machi 2013 chini ya Sir Alex Ferguson (mechi 18).
Huu ni mwendo mrefu wa ushindi kwa Jose Mourinho kwenye mashindano yote (saba) tangu mechi saba mfululizo akiwa na Chelsea Januari 2014.
Zlatan Ibrahimovic tayari amefunga mabao zaidi kwenye mashindano yote kuliko mfungaji bora wa Manchester United msimu uliopita (Martial, 17).
West Ham imepoteza mechi mfululizo kwenye Premier League bila kufunga bao kwa mara ya kwanza chini ya Slaven Bilic.Juan Mata found the net at the London Stadium
Juan Mata alifunga bao London Stadium
Tangu kuanza kwa msimu uliopita, hakuna timu iliyooneshwa kadi nyingi nyekundu kwenye Premier League zaidi ya West Ham (nane - sawa na Southampton).
Juan Mata amehusika katika mabao 40 ya Premier League (mabao 25, assist 15) tangu alipoanza kuichezea Manchester United; wa pili nyuma ya Wayne Rooney katika muda huo (mabao 46 - 29, assist 17).
Kadi nyekundu ya Sofiane Feghouli baada ya dakika 15 ilikuwa kadi nyekundu ya haraka zaidi kwenye Premier League msimu huu. 
Mike Dean ameonesha kadi nyekundu 14 kwenye Premier League tangu mwanzo wa msimu uliopita; sita zaidi ya mwamuzi yeyote.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.