Online

Thursday, January 5, 2017

EPL: Tottenham 2-0 Chelsea: Dele Alli aiwekea 'mwichi' Chelsea kuweka rekodi EPL

Tottenham ilizima jaribio la Chelsea kuweka rekodi kwenye historia ya Premier League kwa ushindi mara 14 mfululizo wakiwachapa mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa White Hart Lane.
Spurs ilipaa hadi nafasi ya tatu katika msimamo kufuatia mabao mawili ya kichwa yaliyofungwa na Dele Alli kuifanya Chelsea kuongoza kwa pointi tano juu ya Liverpool.
Alli aliunganisha krosi ya Christian Eriksen kuiandikia Spurs bao la kuongoza kisha wawili hao wakacheza vizuri na kupata bao la pili dakika ya 54.
Eden Hazard alikosa nafasi mbili kwa Chelsea katika kila kipindi lakini Spurs waligangamala na kuibuka na ushindi muhimu huku wakiwatoa mahasimu wao wa London Kaskazini Arsenal nje ya top four huku wenyewe wakiwa pointi saba nyuma ya vinara wakishinda mara tano mfululizo.

Spurs na rekodi nzuri ya nyumbani - dondoo

  • Chelsea haijashinda White Hart Lane tangu ushindi wa mabao 4-2 Oktoba 2012 (ikitoka sare mbili na kupoteza mbili tangu hapo).
  • Tottenham haijafungwa White Hart Lane msimu huu, ikishinda mara nane na sare mbili; rekodi yao nzuri kwenye msimu wa Premier League kwa mechi za nyumbani tangu 2000-01 (mechi 13).
  • Spurs haijapoteza London derby kwenye Premier League iliyopigwa White Hart Lane chini ya Mauricio Pochettino (ikishinda nane na sare nne).
  • Tottenham ilifunga kwa mashuti mawili yaliyolenga lango kwenye mchezo huu.
  • Dele Alli ameifikia rekodi yake ya 2015-16 ya mabao 10. Ameweza kufanya hivi kwenye mechi 19 msimu huu, ukilinganisha na mechi 33 msimu uliopita.
  • Spurs haijapoteza mchezo wa Premier League ambao Alli amefunga (mechi 16 - ikishinda 12, sare nne).
  • Viungo pekee kufikisha mabao 20 ya Premier League haraka zaidi ya Alli (mechi 52) ni Rafael van der Vaart (44) na Matt Le Tissier (50)
  • Ni Mesut Ozil (22) pekee ana assist nyingi za Premier League tangu mwanzo wa msimu wa 2015-16 zaidi ya Christian Eriksen (20).
  • Hii ilikuwa mara ya nne msimu huu kwenye Premier League ambapo Diego Costa ameshindwa kufunga au kutoa assist.

Kifuatacho?

Tottenham itacheza na Aston Villa kwenye FA Cup raundi ya tatu Jumapili kabla ya kuendelea na kampeni yao ya ligi nyumbani kwa West Brom Jumamosi 14 Januari.
Chelsea watakuwa na Peterborough kwenye FA Cup Jumapili kabla ya kusafiri kuwafuata mabingwa watetezi wa Premier League Leicester siku sita baadaye.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.