Online

Thursday, January 19, 2017

FA Cup: Plymouth Argyle 0-1 Liverpool: Reds wasonga mbele raundi ya nne

Lucas Leiva alifunga bao lake la kwanza baada ya miaka saba na kuipeleka Liverpool hatua ya nne katika FA Cup wakiifunga Plymouth bao 1-0.
Vijana wa Jurgen Klopp walitembea umbali wa maili 293 hadi katika dimba la Home Park baada ya sare ya 0-0 katika mchezo uliopigwa Anfield.
Hata hivyo, Lucas aliihakikishia Reds kuwa hawakupoteza safari hiyo ndefu baada ya kufunga kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona iliyopigwa na Philippe Coutinho mapema kipindi cha kwanza.
Kutokana na ushindi huo, sasa Liverpool itacheza na dhidi ya Wolverhampton Wanderers 28 Januari katika dimba la Anfield.
Kwingineko katika FA Cup, Newcastle United imefuzu raundi ya nne baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Birmingham huku Southampton nayo ikikata tiketi kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Norwich City.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.