Online

Tuesday, January 10, 2017

Kombe la Dunia: Fifa kuongeza timu hadi kufikia 48 katika fainali za Kombe la Dunia

MASHINDANO ya Kombe la Dunia yataongezwa washiriki hadi kufikia 48, kutoka 32, Fifa imeamua.
Hatua ya mwanzo ya makundi ya timu 16 yenye timu tatu zitasonga mbele hatua ya mtoano kwa timu 32 zitakazosalia ambapo mabadiliko hayo yataanza kufanya kazi katika fainali za mwaka 2026.
Chombo chenye mamlaka ya soka la dunia lilipiga kura mabadiliko hayo katika mkutano uliofanyika mjini Zurich.
Idadi ya mechi za mashindano zitaongezeka hadi kufikia 80, kutoka 64, lakini ajabu ni kuwa washindi watacheza mechi saba pekee.
Mashindano hayo yatafanyika ndani ya siku 32 - jaribio la kuzipunguzia klabu kubwa barani Ulaya, ambazo ziliomba mabadiliko kwa sababu ya wingi wa ratiba za kimataifa.
Mabadiliko hayo yanakuja kwa mara ya kwanza tangu mabadiliko yaliyofanywa katika Kombe la Dunia mwaka 1998.

Kwa nini yameongezwa?

Rais wa Fifa Gianni Infantino amekuwa nyuma ya hili, akisema Kombe la Dunia linatakiwa kuwa "mjumuiko zaidi".
Akizungumza katika mkutano wa michezo Dubai Disemba, Infantino alisema uongezaji huo pia utanufaisha "maendeleo ya mchezo huo duniani kote".
Aliongeza: "Hakuna chochote kikubwa katika kuinua soka kwenye nchi zaidi ya kushiriki kwenye Kombe la Dunia."
Licha ya kusema "maamuzi hayo hayatakiwi kuendeshwa kibiashara", Infantino amebainisha uwezekano wa kuongeza fedha.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Fifa yenyewe, pato linatabiriwa kuongezeka hadi paundi 5.29bn kwa mashindano ya timu 48, yakitoa faida ya paundi 521m.

Historia ya mabadiliko katika Kombe la Dunia

Kombe la DuniaTimuMuundo
1930 Uruguay13Kundi 1 la timu 4 na makundi 3 timu 3, vinara walifuzu nusu-fainali
1934 Italia16Moja kwa moja hatua ya mtoano
1950 Brazil15 (ingawa timu 13 zilishiriki)Makundi 3 ya timu 4 na kundi 1 timu 3, ambapo vinara walifuzu hatua ya mwisho ya kundi la timu nne
1954 Switzerland16Makundi 4 ya timu 4, lakini mechi 2 kwa kila kundi, ambapo timu 2 za juu zilitinga robo-fainali
1958 Sweden16Makundi 4 ya timu 4, mara hii zilicheza mechi 3. Timu 2 za juu zilifuzu hatua ya robo-fainali
1974 Ujerumani Magharibi16Makundi 4 ya timu 4 lakini sasa yalifuatiwa na makundi 2 ya timu 4, timu 2 za juu zilicheza fainali
1982 Uhispania24Makundi 6 ya timu 4 yakafuatiwa na makundi 4 ya timu 3, mshindi wa kila kundi alifuzu nusu-fainali
1986 Mexico24Makundi 6 ya timu 4, timu 2 za juu na 4 za nafasi ya 3 zilifuzu hatua ya 16
1998 Ufaransa32Makundi 8 ya timu 4, timu 2 za juu zilisonga mbele hatua ya mtoano

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.