Online

Monday, January 23, 2017

La Liga: Eibar 0-4 Barcelona: Barca yaongeza presha kwa Real Madrid

MABINGWA watetezi Barcelona waliendelea kuiongezea presha mahasimu wao katika soka la Uhispania Real Madrid na Sevilla baada ya ushindi wa mabao 4-0 ugenini dhidi ya Eibar.
Mchezaji wa akiba Denis Suarez, ambaye alichukua nafasi ya majeruhi Sergio Busquets, alifunga bao la kuongoza, kabla ya Barca kuongeza presha baada ya mapumziko, wakifunga bao la pili kupitia kwa Lionel Messi aliyemalizia pasi ya Luis Suarez.
Luis Suarez akamzidi ujanja mlinzi Florian Lejeune na kufunga bao la tatu kabla ya Neymar kufunga bao la nne.
Ushindi huo unaifanya Barca inayokamata nafasi ya tatu kuwa nyuma ya vinara Madrid kwa pointi mbili, na pointi moja nyuma ya Sevilla.
Madrid - ambayo iliichapa Malaga mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa Bernabeu Jumamosi - wana mchezo mmoja mkononi, baada ya kuukosa mwezi Disemba walipokuwa kwenye fainali za Club World Cup.
Kwingineko kwenye La Liga, Sevilla iliendelea kuibana Madrid baada ya kuichapa Osasuna mabao 4-3, huku Athletic Bilbao ikilazimishwa sare ya mabao 2-2 nyumbani na Atletico Madrid. Real Betis ikatoka sare ya 0-0 na Sporting Gijón na Real Sociedad ikaichapa Celta Vigo bao 1-0.

Kifuatacho?

Kurejea kwenye Copa del Rey kwa timu zote. Mabingwa watetezi Barcelona wataialika Real Sociedad Alhamisi wakiwa na faida ya bao 1-0 katika hatua ya robo-fainali.
Eibar, wakicheza robo-fainali yao ya kwanza, watajaribu kurejesha kipigo cha mabao 3-0 walichopigwa na Atletico Madrid Jumatano.
Kwenye mechi nyingine mbili, Real Madrid watakuwa na kibarua kigumu cha kupindua kipigo cha mabao 2-1 watakapoitembelea Celta Vigo na Alaves walianza na ushindi wa mabao 2-0 nyumbani watakuwa na Alcorcon.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.