Online

Monday, January 30, 2017

La Liga: Real Madrid 3-0 Real Sociedad: Real yaongoza La Liga kwa pointi nne zaidi

Real Madrid ilipata faida ya Barcelona na Sevilla kupoteza pointi muhimu wakiichapa Real Sociedad mabao 3-0 na kuongoza msimamo wa La Liga kwa pointi nne zaidi huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi.
Wenyeji walitangulia kufunga baada ya Cristiano Ronaldo kumtengenezea Mateo Kovacic kufunga bao lake la kwanza la La Liga.
Naye Kovacic akatoa assist kwa Ronaldo aliyefunga bao la pili akimzidi ujanja mlinda mlango Geronimo Rulli - likiwa bao lake la 13 katika mechi 13.
Wageni wakamkosa Inigo Martinez ambaye alitolewa nje kwa kadi mbili za manjano kabla ya Alvaro Morata kufunga kwa kichwa bao la tatu akimalizia krosi ya Lucas Vazquez
Kwingineko kwenye La Liga, Real Betis iliibana Barcelona na kutoka sare ya bao 1-1 huku Espanyol ikiitandika Sevilla mabao 3-1 na Ath Bilbao wakiichapa Sporting Gijón mabao 2-1.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.