Online

Sunday, January 8, 2017

La Liga: Real Madrid 5-0 Granada: Isco apiga mbili Madrid ikiifikia rekodi ya Barcelona

VINARA wa La Liga Real Madrid wameifikia rekodi ya Barcelona katika soka la Uhispania ya mechi 39 mfululizo bila kupoteza wakiichapa Granada mabao 5-0.
Vijana wa Zinedine Zidane walikuwa mbele kwa mabao 4-0 ndani ya dakika 32, ambapo Isco alitangulia kufunga akimalizia pasi ya Karim Benzema.
Benzema akafunga bao la pili baada ya Guillermo Ochoa kushindwa kuokoa shuti la Luka Modric, kabla ya Cristiano Ronaldo kufunga bao la tatu.
Isco akafunga bao la nne akimalizia krosi ya Modric, na kiungo Casemiro akafunga bao la tano akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na James Rodriguez.
Kwingineko kwenye La Liga, Atletico Madrid iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Eibar huku Las Palmas wakiichapa Sporting Gijón bao 1-0 na Real Sociedad wakilala kwa mabao 4-0 kutoka kwaa Sevilla.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.