Online

Thursday, January 26, 2017

League Cup: Liverpool 0-1 Southampton (0-2): Southampton yatangulia Wembley

Southampton imekuwa timu ya kwanza kutinga fainali ya EFL Cup itakayopigwa Wembley kwa ushindi wa bao 1-0 katika mechi zote mbili za nusu-fainali dhidi ya Liverpool - wakishinda mechi ya pili kwa bao la Shane Long dakika za lala salama katika dimba la Anfield.
Vijana wa Claude Puel, walikuwa na faida ya bao 1-0 walilolipata kwenye mchezo wa kwanza, walikaribia kuwafunga mapema Liverpool ndani ya dakika 45 za kwanza lakini shuti la Dusan Tadic liliokolewa na mlinda mlango wa Reds Loris Karius huku nahodha Steve Davis akipiga shuti lililokosa uelekeo.
Liverpool walipoteza nafasi mbili za wazi kupitia kwa Daniel Sturridge, huku mlinda mlango wa Southampton Fraser Forster akiokoa kwenye mstari shuti la Emre Can huku Liverpool wakinyimwa penalti dakika za lala salama baada ya mchezaji wa akiba Divock Origi kuangushwa na Jack Stephens.
Southampton wakamaliza kazi kupitia kwa Long aliyefunga akimalizia pasi ya Josh Sims na kuwafanya watinge fainali yao ya kwanza katika mashindano haya tangu 1979, ambapo watakutana na ama Manchester United au Hull City - hatua waliyofikia bila kuruhusu bao.

Dondoo muhimu kuzifahamu...

  • Hii ni mara ya kwanza kwa Jurgen Klopp kupoteza mchezo wa nusu-fainali akiwa kama meneja, akifuzu katika nusu-fainali sita zilizopita.
  • Southampton imetinga fainali bila kufungwa hata bao moja.
  • Liverpool imeshindwa kufunga bao katika michezo yote mitatu v Southampton msimu huu katika mashindano yote.
  • Claude Puel hajafungwa kwenye mechi sita dhidi ya Liverpool akiwa meneja (W3 D3).
  • Hii ni mara ya pili Liverpool kuondolewa kwenye nusu-fainali sita za League Cup (nyingine ilikuwa v Chelsea msimu wa 2014-15).
  • Mara ya mwisho kwa Liverpool kushindwa kufunga kwenye mechi zote mbili za nusu-fainali ilikuwa msimu wa 1970-71 kwenye Fairs Cup v Leeds.

Kifuatacho?

Liverpool itawaalika Wolves kwenye mchezo wa FA Cup raundi ya nne Jumamosi, wakati Southampton watakuwa njiani kuwafuata Arsenal kwenye mashindano hayo.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.