Online

Wednesday, January 11, 2017

League Cup: Manchester United 2-0 Hull City: Mourinho atanguliza mguu mmoja fainali EFL Cup

Jose Mourinho ametanguliza mguu mmoja kuelekea taji lake la kwanza katika msimu wa kwanza kuwa meneja wa Manchester United baada ya mabao ya Juan Mata na Marouane Fellaini kuipa timu hiyo ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Hull City kwenye nusu-fainali ya kwanza ya EFL Cup.
Licha ya kufungwa lakini wageni hao walikuwa na nafasi kadhaa dhidi ya timu ambayo imeshinda mara nane mfululizo kwenye mashindano yote, Robert Snodgrass akisababisha tafrani katika lango la wenyeji.
Hata hivyo, Mata alifunga bao la kuongoza akimalizia kazi nzuri ya Henrikh Mkhitaryan kabla ya mchezaji wa akiba Fellaini kufunga bao la pili, akiunganisha kwa kichwa krosi ya Matteo Darmian na kuiwekea mazingira mazuri United kuelekea mchezo wa marudiano 26 Januari.

Red Devils yaendeleza ushindi - dondoo

  • Manchester United imeshinda mechi tisa mfululizo kwenye mashindano yote, rekodi yao nzuri tangu mechi 11 Februari 2009.
  • Juan Mata amefunga kwenye mechi tatu kati ya nne za League Cup (mabao mawili akiwa na Manchester United, moja akiwa na Chelsea).
  • Assist zote za tatu za Henrikh Mkhitaryan akiwa na Manchester United ametoa kwenye EFL Cup.
  • Marouane Fellaini amefunga bao lake la kwanza la League Cup tangu Agosti 2013 (Everton v Stevenage).
  • The Red Devils imesonga mbele katika nusu-fainali zote tatu za League Cup zilizopita ambazo ilishinda mechi ya kwanza (1983 v Arsenal, 1991 v Leeds, 1994 v Sheffield Wednesday).
  • United imeshinda mara 12 na haijapoteza mchezo katika mechi 13 dhidi ya Hull City kwenye mashindano yote (D1).
  • The Red Devils imepoteza mara moja pekee katika mechi 26 za League Cup ilizocheza nyumbani dhidi ya timu-mwenza kwenye Premier League (W24 D1), ilichapwa mabao 2-1 dhidi ya Chelsea Januari 2005.
  • Hull imeshindwa kufunga kwenye kila mchezo katika mechi nne ilizocheza na United, ikipoteza tatu na sare moja.

Kifuatacho?

Marejeo ya Premier League kwa Manchester United ambapo watakutana na vijana wa Jurgen Klopp Liverpool Jumapili ikifahamu ushindi utawapeleka tano bora.
Hull, wakati huo huo, itaialika Bournemouth wakijaribu kujinasua kutoka mkiani mwa msimamo. The Tigers haijashinda kwenye ligi tangu 6 Novemba.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.