Online

Thursday, January 12, 2017

League Cup: Southampton 1-0 Liverpool: The Saints mguu mmoja ndani kuelekea Wembley

Southampton ilipata faida katika mchezo wa kwanza wa nusu-fainali ya EFL Cup wakiichapa Liverpool bao 1-0 katika mchezo uliopigwa St Mary's.
Nathan Redmond alifunga bao pekee akimalizia pasi ya Jay Rodriguez kuipa Saints faida pindi watakapocheza mchezo wa marudianoAnfield 25 Januari - lakini Southampton wanaweza kupoteza bahati ya kucheza fainali itakayopigwa Wembley.
Mlinda mlango wa Liverpool Loris Karius alikuwa mmoja wa wachache katika kikosi cha Jurgen Klopp walioonesha kiwango kizuri, akiokoa mara mbili hatari kutoka kwa Redmond.

Dondoo

  • Baada ya kupoteza mechi nne kati ya tano dhidi ya Liverpool (D1), Southampton sasa hawajafungwa kwenye mechi tatu dhidi ya Reds (W2 D1).
  • Claude Puel hajafungwa kwenye mechi nne dhidi ya Liverpool akiwa meneja (W2 D2).
  • Liverpool ilipiga mashuti mawili pekee yaliyolenga lango katika mechi zote dhidi ya Southampton msimu huu - ni dhidi ya Man City pekee (moja) walipiga mashuti machache msimu huu.
  • Jay Rodriguez alitoa assist yake ya kwanza kwenye mashindano yote akiwa na Southampton tangu Januari 2014 dhidi ya Arsenal.
  • Southampton imekuwa na clean sheet nyingi zaidi ya timu yoyote kwenye EFL Cup msimu huu (nne).

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.